JESHI la Polisi Mkoa wa Pwani limekusanya Sh bilioni 2.2 kutokana na faini za papo kwa papo kutokana na makosa ya usalama barabarani katika kipindi cha miezi mitatu iliyopita.




























Akizungumza na waandishi wa habari mjini Kibaha, Kamanda wa Polisi wa mkoa huo, Salim Morcase alisema fedha hizo zilizotokana na faini walizopigwa madereva kwenye maeneo mbalimbali.
Morcase alisema kuwa, waliweza kukamata makosa 74,446 ambayo yalifanywa na madereva na kupigwa faini za papo hapo katika kipindi hicho cha Septemba hadi Novemba mwaka huu.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo





