Mamlaka: Mwandishi usifanye haya, yatakugharimu Uchaguzi Mkuu

Jeshi la Polisi Nchini limewataka waandishi wa habari waliopangwa kuripoti habari za uchaguzi kutumia akili zao kwa kuangalia usalama wao kwanza pindi Jeshi la Polisi linapotekeza maagizo yake katika kipindi hiki cha uchaguzi, anaripoti Rachel Balama (Diramakini) Dar es Salaam.

Kauli hiyo imetolewa na Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Makao Makuu, ACP Mayala Towo
wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kwenye kikao kilichowakutanisha waandishi wa habari , wawakilishi kutoka NEC ulioandaliwa na Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA).

Amesema kuwa, pale inapotokea vurugu au fujo askari hawatakuwa na muda wa kuangalia kama ni waandishi au la isipokuwa wao watatekeleza maagizo waliopewa.

"Waandishi ni vyema pale inapotokea fujo au vurugu kwenye maeneo mliopangwa siku ya kupiga kura ni vizuri kutumia akili zenu kwa kujali usálama wenu kwanza kwani askari watakapotekeleza amri hawawezi kujua kama wewe ni mwandishi au la,"amesema.

Ameongeza kuwa inapotokea tatizo askari utoa tahadhari mara tatu hivyo kama mwandishi unatakiwa kuangalia na kujali usalama wako hivyo unaweza kukimbia ili kujiepusha na na tatizo ambalo linaweza kukupata pindi askari wanapotekeleza agizo.

Kwa upande wake Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Habari na Elimu kwa mpiga kura kutoka NEC, Dkt. Cosmas Mwaisobwa amesema, NEC imetoa Vitambulisho kwa waandishi wa habari ili kuripoti habari za uchaguzi, lakini vitambulisho hivyo haviwaruhusu wao kuingia ndani ya kituo.

Amesema kuwa, sheria imetaja wanaoruhusiwa kuingia ndani ya vituo lakini waandishi wa habari hawajatajwa hivyo hawaruhusiwi kuingia ndani isipokuwa wao wataripoti yanayoendelea kwa nje

Naye Mkurugenzi Mkuu wa TCRA,Mhandisi James Kilaba amewataka waandishi wa habari kutotangaza matokeo na badala yake yake watekeleze wajibu wao.

Amesema kuwa, kwa mujibu wa sheria anayeruhusiwa kutangaza matokeo anajulikana hiyo kazi ya Mwandishi ni kuripoti habari kutoka kwenye vyanzo sahihi na si vinginevyo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here