Nabii Msigwa aongoza maombi ya kuombea Uchaguzi Mkuu

Mtume na Nabii Richard Msigwa wa Huduma ya Ebenezer Deliverance Ministry (EDM) iliyopo Baruti Manispaa ya Musoma Mkoa wa Mara ameongoza maombi maalumu kanisani kwake  ya kuombea Uchaguzi Mkuu unaotarajia kufanyika Oktoba 28 mwaka huu, huku akiwataka Watanzania wote kuhakikisha wanadumisha amani na utulivu, anaripoti Amos Lufungulo (Diramakini) Mara.
Nabii Msigwa  ameyasema hayo kanisani hapo ikiwa ni siku ya pili ya maombi yanayofanywa na huduma hiyo chini yake na waumini wa Huduma ya  Ebenezer ambapo yatahitimshwa leo kwa lengo la kumuomba Mungu awezeshe zoezi la uchaguzi liweze kufanyika kwa amani katika kuwachagua madiwani,wabunge na Rais.

Ameongeza kuwa, tangu mwanzo watawala walikuwepo na walichaguliwa na Mungu. Hivyo akasisitiza kuwa Mungu pekee ndiye mwenye uwezo wa kuwaongoza Watanzania kuchagua viongozi bora watakaotenda haki na kuwaletea maendeleo Watanzania kama ambavyo miaka mitano imekuwa ya neema na baraka kwa mafanikio makubwa Kktika nyanja za kijamii na kiuchumi na ndio maana huduma hiyo imechukua jukumu la kuombea uchaguzi huo.

"Kupitia maombi yetu, Mungu atatuwezesha kupata viongozi bora wenye hofu ya Mungu na watakao tenda haki, tunataka viongozi watakaochaguliwa katika uchaguzi huu watokane na Mungu na siyo waganga wa kienyeji, tunauhakika Mungu atasikia maombi yetu na kujibu sawa sawa na tulivyo muomba,"amesema Nabii Msigwa.

Aidha, Nabii Msigwa amewataka watanzania wote kudumisha amani na utulivu katika kipindi chote cha uchaguzi. Ambapo amesisitiza kuwa amani ndiyo msingi na chimbuko la maendeleo katika Taifa, hivyo ameonya wenye kuchezea amani wasifanye hivyo hata kidogo bali wailinde amani na kuitunza kama amabvyo Mungu ameagiza kwenye kitabu Kitakatifu yaani Biblia.
 
"Tunahubiri injili kwa sababu ya amani, Watanzania wanafanya kazi za maendeleo yao kwa sababu ya amani, tuilinde amani yetu kwa maslahi yetu sote Mungu ametupa Taifa ambalo misingi yake ni ya kupendana, kuthaminiana na kujaliana kupitia maombi haya tunaamini Mungu atasimama na Tanzania na kuivusha salama kipindi hiki cha Uchaguzi Mkuu na hata baada ya uchaguzi kufanyika,"amesema Nabii Msigwa.
Pichani Mtume na Nabii Richard Msigwa wa Huduma ya Ebenezer  Deliverance Ministry ( EDM) iliyopo Baruti Musoma akioongoza maombi ya kuombea Taifa kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28, mwaka huu. (Picha na EDM).

Ametoa wito pia kwa viongozi wa dini na Watanzania wote, kuendelea kuombea amani na utulivu katika kipindi hiki kilichosalia kabla ya uchaguzi kufanyika, huku akibainisha kuwa kama ambavyo Mungu amesaidia kulivusha Taifa katika janga la Corona na uchaguzi utafanyika kwa amani na utulivu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here