Msajili wa Vyama vya Siasa naye afunguka

"Sisi hapa tukianzisha vurugu tuna uwezo wa kupanda ndege, habari gani kuhusu wengine ambao hawana hili wala lile. Vipi kuhusu watoto na makundi mengine;

Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji Mstaafu Francis Mutungi ameyasema hayo leo Oktoba 2,2020 ambapo amewataka wadau wote wa uchaguzi wakiwemo wanasiasa kuepuka misuguano na Serikali, anaripoti Mwandishi Diramakini (diramakini@gmail.com).
 
Jaji Mutungi katika kikao hicho cha pamoja na wadau wote wa siasa kilichofanyika jijini Dar es Salaam amesema yeye kama mlezi wa vyama vya siasa hafurahishwi na baadhi ya kauli za vyama vya siasa kupitia wagombea wao.

Amesema, kauli hizo ni wazi zinaenda kinyume na kanuni za maadili ya uchaguzi walizosainishwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), hivyo kuwataka kujisahihisha na kutumia siku chache zilizosajilia kunadi sera zao.

Msajili huyo wa vyama amewataka, wadau wote wenye malalamiko yeyote kuhusu uchaguzi wafike NEC kwani ndiyo yenye mamlaka ya kuratibu uchaguzi nchini, hatua ambayo itawawezesha kupata suluhisho la madukuduku yao.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news