Mtendaji Mkuu wa Mahakama Tanzania,Menejimenti Mahakama Kuu wafanya ukaguzi Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bw. Mathias Kabunduguru (aliyenyoosha mkono juu) akielezea jambo mbele ya timu ya mainjinia wakati walipofanya ukaguzi katika moja ya Vituo Jumuishi cha Utoaji haki (IJC) kinachoendelea kujengwa katika Manispaa ya Kinondoni Jijini Dar es salaam. Bw. Kabunduguru alifanya ukaguzi wa jengo hilo Oktoba mosi lengo likiwa ni kujionea maendeleo ya ujenzi.Pichani ni muonekano wa jengo la Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) lilichopo katika ujenzi, jengo linajengwa katika Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Bw. Mathias Kabunduguru akiwa ameambatana na Mkuu wa kitengo cha usimamizi wa Majengo ya Mahakama ya Tanzania Eng. Khamadu Kitunzi (kulia) na Mkurugenzi Mtendaji wa Habconsult Ltd Bw. Habib Nuru (kushoto) wakati wa zoezi la kukaguzi wa jengo la kituo jumuishi cha utoaji haki kinachoendelea kujengwa Manispaa ya Temeke. Mtendaji Mkuu alipata fursa pia ya kukagua jengo la Kituo Jumuishi cha Temeke.Mhandisi kutoka 'Hainan International Ltd' , Eng. Greyson Kampuni inayojenga Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki vya Kinondoni na Temeke akiwaonyesha Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama Kuu ya Tanzania jengo hilo lililopo katika ujenzi, kwa mujibu wa Mhandisi huyo ujenzi wa kituo hicho unatarajiwa kukamilika Desemba mwaka huu, 2020.Wajumbe wa Menejimenti ya Mahakama Kuu ya Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kukagua jengo la 'IJC' linalojengwa katika Manispaa ya Wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.Sehemu ya Maafisa kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania, Naibu Wasajili na Watendaji wakipata maelezo kutoka kwa Mhandisi Greyson pindi walipotembelea kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Kinondoni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news