Rais Shein awaongoza wananchi kupiga kura

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Ali Mohamed Shein amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenda kupiga kura na kuwachagua viongozi wanaowataka na wala wasiwe na hofu kwani Serikali yao imewawekea ulinzi wa kutosha.

Hayo ameyasema leo Oktoba 28,2020 wakati alipofanya mahojiano na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali mara baada ya kumaliza zoezi la kupiga kura huko katika kituo cha kupiga kura Bungi, Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja, ambapo Rais Dkt.Shein alitimiza haki yake hiyo ya msingi mapema subuhi mnamo majira ya saa mbili kaso robo.

Rais Dkt.Shein alifika kituoni hapo akiwa amefuatana na mkewe mama Mwanamwema Shein na mara baada ya kufika wote kwa pamoja walifuata taratibu zote za kupiga kura wakiwa wameanza kwa kupanga foleni katika mistari maalum iliyopangwa.

Katika mahojiano hayo, Rais Dkt.Shein amesema kuwa yeye amepiga kura na kuchukua muda mfupi sana kutokana na taratibu zilizopangwa na kuwataka wananchi kwenda mapema ili na wao wapate fursa ya kuwachagua viongozi wanaowataka baada ya kusikiliza kampeni za vyama vya siasa na kueleza imani yake kwamba anaamini tayari wameshafanya uamuzi.

Amesisitiza kwamba hali ya ulinzi ni nzuri na hali iko shwwari sana hivyo waliwataka wananchi wasiwe na hofu na wala wasiogope kwani leo ndio siku yao ya kufanya maamuzi wanayoyataka.

Ameongeza kuwa, wananchi hawatakiwi kuwa na hofu kwani wako nchini mwao na wako huru na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni Serikali yao kwani wana wajibu wa kuwachagua viongozi wengine wapya baada ya wao kumaliza madaraka.

Rais Dkt.Shein ameeleza kuwa, mtu hatakiwi kuwa na hofu wakati akiwa nchini mwake kwani Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar tayari imewathibitishia wananchi kwamba imewawekea ulinzi wa kutosha.

Sambamba na hayo, Rais Dkt.Shein amewataka wananchi kutochelea kwenda kupiga kura na kuwasisitiza kwamba waende wakapige kura kwa azma ya kutekeleza jukumu lao la msingi huku akisisitiza kwamba ni lazima kila mmoja aende akachague kiongozi anaemtaka.

Rais Dkt.Shein amewataka wananchi waende kupiga kura na wasiwe na dhana zaidi kuliko ukweli na kuwataka wasisikilize hadidthi nyingine zisiso na ukweli kuhusu ukweli uliopo.

“Isijefika wakati mtu akaja kujuta na kubaki akisema mimi sikwenda ninge...ninge, ningejua, kwani ninge haiisaidii na badala yake waende katika vituo vyao wakapinge kura,”amesisitiza Dkt.Shein.

Akitoa nasaha zake kwa mgombea atakaeshinda, katika nafasi zote zinazogombewa, Rais Dkt. Shein amesisitiza haja kwa mgombea kuzingatia katiba ya nchi kwani nchi hii inaongozwa kwa Katiba, Sheria na taratibu zilizowekwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news