Kwa mujibu wa Mail, Meneja wa Chelsea, Frank Lampard yuko tayari kumjumuisha, Antonio Rudiger (27) kwenye mipango yake ya kikosi cha kwanza. Hatua hiyo inatokana na mazungumzo na mlinzi huyo wa kati wa Ujerumani ambaye amekuwa akihusishwa na timu za Tottenham na Paris St-Germain lwa sasa.
Footbal Insider inaripoti kuwa, Crystal Palace imeanza mazungumzo na winga wa Uingereza, Andros Townsend (29) kuhusu mkataba mpya baada ya kufanikiwa kuzima mipango ya West Brom iliyokuwa inamtaka majira ya joto.
Wakati huo huo, Meneja wa West Bromwich Albion F.C, Slaven Bilic amekasirishwa na mtendaji mkuu wa Baggies baada ya kumruhusu mlinzi wa Misri, Ahmed Hegazi (29) kuondoka na kujiunga na Al-Ittihad inayoshiriki Ligi Kuu ya Saudi Arabia bila yeye kujua.
Aidha, Tottenham wanatarajia kufikia makubaliano ya kusitisha mkataba wa mlinzi wa kushoto raia wa Uingereza, Danny Rose (30) hii ikiwa ni kwa mujibu wa Football Insider,nyota huyo anatarajia kulipwa zaidi ya Euro 2.5milioni ya thamani ya mkataba wake uliobaki ambao unafikia tamati Juni, 2021.
Kwa upande wa Mail,Bodi ya Ligi Kuu England itajiweka kando katika juhudi zake za kuishawishi Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi hiyo kuleta visa maalumu, baada ya Engalnd kujiondoa rasmi Umoja wa Ulaya.

![]() |
| Danny Rose. (Getty Images). |