Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo Oktoba 26,2020.Upepo wa Pwani unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya kilomita 30 kwa saa kwa Pwani yote kutoka Kusini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Mashariki kwa Pwani ya Kusini.
MCHAMBUZI NI THEREZA NGASSA
Kwa mujibu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA), maeneo ya mikoa ya Ziwa Victoria pamoja na Magharibi mwa nchi yanatarajiwa kuwa na hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

