CHADEMA yawakana wabunge 19 walioapishwa leo

Muda mfupi baada ya Wabunge 19 wa Viti Maalum wa Chama cha Demokrasaia na Maendeleo (CHADEMA) kuapishwa katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma, chama hicho kimewakana, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Walioapishwa ni Mwenyekiti wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Taifa (BAWACHA),Halima Mdee, Felister Njau, Nagenjwa Kaboyoka, Sophia Mwakagenda, Kunti Majala, Stella Fiao, Anatropia Theonest, Salome Makamba, Conchesta Rwamlaza,Grace Tendega, Esther Matiko, Cecilia Pareso, Ester Bulaya, Agnesta Lambart, Nusrati Hanje, Jesca Kishoa, Hawa Mwaifunga, Tunza Malapo na Asia Mohammed.
 
Katibu Mkuu wa CHADEMA, John Mnyika amesema hawatambui orodha ya wabunge wa chama hicho wa viti maalum walioapishwa na Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheushimiwa Job Ndugai jijini Dodoma leo.
Amesema, Kamati Kuu ya chama hicho ndio hukaa na kupitisha majina hayo, lakini haijafanya hivyo, hata mchakato wa kuyapeleka majina ya wabunge wa viti maalum wa chama hicho Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) pia amedai haukufanyika.

Post a Comment

0 Comments