Chama hana mpango na Yanga SC

Nyota wa Klabu ya Simba, Clatous Chama ameweka wazi kuwa mpango wake wa sasa ni kuitumikia timu hiyo na hana mpango wa kuibukia ndani ya Yanga SC.
Hayo ni kwa mujibu wa chanzo cha karibu na nyota huyo ambacho kimeidokeza Diramakini na tayari awali uongozi Simba SC uliibuka na msimamo kuwa kiungo wao huyo kamwe hawezi kujiunga na watani zao wa jadi Yanga hata kama wataamua kumtangazia dau kubwa zaidi.
 
Siku za karibuni habari zimekuwa zikieleza kuwa Klabu ya Yanga ipo kwenye mpango wa kuinasa saini ya nyota huyo raia wa Zambia.

Nyota ambaye ana tuzo ya mchezaji bora kwa msimu wa 2019/20 baada ya kutoa jumla ya pasi 10 na kufunga mabao mawili kati ya 78 yalifungwa na Simba.

Kwa sasa Chama mwenye pasi tano na mabao mawili kati ya 22 yaliyofungwa na Simba yupo zake nchini Zambia na timu ya Taifa ambayo jana Novemba 12 ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Botswana kwenye mchezo wa kufuzu Afcon.
Rais wa Zambia, Mheshimiwa Edgar Lungu akifuatilia mchezo huo jana.

Post a Comment

0 Comments