Mwenyekiti wa AAPAM Tawi la Tanzania , Bi. Leila Mavika, ametangaza kufanyika kwa Mkutano Mkuu wa Pili wa Mwaka wa Jumuiya ya Wataalamu wa Usimamizi wa Rasilimaliwatu na Utawala katika Utumishi wa Umma, utakaoanza Mei 5 hadi 8, 2026 jijini Arusha.
Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 28, 2026, Bi. Mavika amesema mkutano huo unalenga kuwakutanisha wataalamu wa utawala wa umma na usimamizi wa rasilimaliwatu ili kujadili mbinu bora za kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari Aprili 28, 2026, Bi. Mavika amesema mkutano huo unalenga kuwakutanisha wataalamu wa utawala wa umma na usimamizi wa rasilimaliwatu ili kujadili mbinu bora za kuboresha utendaji kazi na utoaji wa huduma kwa wananchi.Amesema mkutano huo utaongozwa na kaulimbiu isemayo “Kufikiri upya utoaji wa huduma kwa Umma: Jinsi Serikali inavyoweza kutumia Teknolojia kuanzisha huduma bora na zinazolenga wananchi, kukabiliana na ukosefu wa ajira kwa vijana na changamoto za mazingira.”
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo


















