Matiko naye afunguka mazito baada ya kuapishwa bungeni

Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ester Matiko amesema kuwa, hatua ya leo Novemba 24, 2020 ya kufika mbele ya Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai kuapishwa ni matokeo ya baraka zote kutoka ndani ya chama baada ya kuyabariki majina yao, anaripoti Mwandishi Diramakini.

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akimwapisha Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Esther Matiko kwenye viwanja vya Bunge jijini Dodoma leo Novemba 24, 2020.

“Kama mnavyofahamu mchakato wa kupata wabunge wa Viti Maalum ni mrefu,unaanzia kwenye Baraza la Wanawake,baadaye chama kikibariki yanenda NEC (Tume ya Taifa ya Uchaguzi).Mimi mpaka kufika hapa nimetaarifiwa na mamlaka husika,"amesema Matiko.

Bi.Matiko ambaye kabla ya alikuwa Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini amewaondoa hofu wanachama wa chama hicho, kwa madai kuwa, licha ya uchache wao wategemee mambo tofauti bungeni. "Pia sisi hatupo kwa ajili ya chama, tupo kwa ajili ya kuwatumikia wananchi,"amesema wakati akitoa ufafanuzi iwapo watafukuzwa ndani ya chama.

Post a Comment

0 Comments