Ngorongoro Heroes yawapa heshima Watanzania

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imepata heshima ya kipekee katika soka baada ya vijana chini ya umri wa miaka 20 wa timu ya Ngorongoro Heroes kuwapa tabasamu Watanzania,anaripoti Mwandishi Diramakini.

Ni baada ya kufuzu kwenda fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kwa vijana chini ya umri wa miaka hiyo, kutokana na ushindi wa 1-0 dhidi ya Sudan Kusini.

Matokeo hayo ya Novemba 30, 2020 yamewapa nguvu na ujasiri Watanzania kupitia mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Black Rhino Academy mjini Karatu katika Jiji la Arusha.

Kassim Haruna ndani ya dakika ya 56 kwa kushirikiana na wenzake ndiye aliyewezesha bao hilo ambalo limetoa faraja kwa wengi.

Aidha, kwa sasa, timu hiyo itacheza na Uganda Jumatano hii katika fainali baada ya kuitoa Kenya.

Katika Nusu Fainali ya kwanza, The Kobs waliichapa Kenya 3-1 katika Uwanja wa Black Rhino Academy uliopo Karatu, Arusha.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news