Jeshi la Polisi lafanikiwa kupunguza makosa makubwa kwa asilimia 15.5

 

Jeshi la Polisi nchini limefanikiwa kupunguza makosa makubwa ya jinai kwa Asilimia Kumi na Tano Pointi Tano katika Kipindi cha Mwaka 2020 ambapo matukio yaliyoripotiwa katika vituo mbalimbali nchini ni 50,689 tofauti na mwaka 2019 ambapo matukio yaliyoripotiwa ni 58,590 huku hali ya nchi ikibakia salama na wananchi wakiendelea na shughuli za kujenga uchumi.
Hayo yamesemwa na Inspekta Jenerali wa Polisi nchini, Simon Sirro wakati wa ziara ya Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Khamis Hamza Chilo alipotembelea Makao Makuu ya Jeshi hilo leo, jijini Dodoma.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo kwa niaba ya Serikali,Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Khamis Hamza Chilo amelipongeza jeshi hilo kwa kazi wanayofanya ya kusimamia amani na usalama nchini huku akiwataka kuongeza juhudi katika utendaji wao.

Post a Comment

0 Comments