Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) limekifungia kiwanda cha SAN SHAN na BAI-LY PAPER CO. LTD kwa kukiuka sheria na taratibu za mazingira, hatua iliyochukuliwa baada ya timu ya ukaguzi wa mazingira uliofanyika katika Wilaya ya Mkuranga ukiongozwa na Meneja wa Utekelezaji wa Sheria wa NEMC, Mhandisi Luhuvilo Mwamila.


Akizungumza baada ya ukaguzi huo, Mhandisi Luhuvilo alisema kiwanda cha SAN SHAN kinachojihusisha na uchakataji wa mafuta machafu (waste oil) kimekuwa kikizalisha moshi mzito na harufu kali kutokana na kukosa mfumo wa kudhibiti hewa chafuzi.
Aidha, kiwanda hicho kimekuwa kikitiririsha maji taka yenye mafuta machafu kwenye mazingira na kusababisha uchafuzi mkubwa katika maeneo ya jirani.














Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo



