Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today January 21st, 2021

  Utabiri wa hali ya hewa wa saa 24 zijazo kuanzia saa 3:00 usiku wa leo Januari 21, 2021 unawasilishwa na Doreen Mwara kutoka Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania (TMA).

 
UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO: TAREHE: 21/01/2021.

Mikoa ya Ruvuma, Kusini mwa mkoa wa Morogoro, Songwe, Mbeya, Rukwa, Iringa, Njombe, Lindi na Mtwara: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu, mvua na ngurumo katika baadhi ya maeneo na vipindi vifupi vya jua.

..........

Mikoa ya Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Kigoma, Tabora, Katavi, Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro, Dodoma na Singida: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.

...........

Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Tanga pamoja na Visiwa vya Unguja na Pemba: Vinatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.

............

Mikoa ya Kilimanjaro, Manyara na Arusha: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.

..........

ANGALIZO

1. VIPINDI VIFUPI VYA MVUA KUBWA VINATARAJIWA KATIKA BAADHI YA MAENEO YA MIKOA YA LINDI, MTWARA, KUSINI MWA

MKOA WA MOROGORO, MBEYA, SONGWE, IRINGA, NJOMBE NA RUVUMA.

2. VIPINDI VYA UPEPO MKALI UNAOFIKIA KM 40 KWA SAA NA MAWIMBI MAKUBWA YANAYOFIKIA MITA 2 VINATARAJIWA

KATIKA BAADHI YA MAENEO YA UKANDA WA PWANI YOTE YA BAHARI YA HINDI (MIKOA YA TANGA, DAR ES SALAAM,

PWANI (IKIJUMUISHA VISIWA VYA MAFIA), LINDI NA MTWARA PAMOJA NA VISIWA VYA UNGUJA NA PEMBA).


VIWANGO VYA JOTO KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:

MJI              Kiwango cha juu   Kiwango cha chini  

                    cha joto                cha joto

ARUSHA       29°C                    15°C

D'SALAAM   32°C                     24°C

DODOMA    28°C                     20°C

KIGOMA      28°C                     20°C

MBEYA         26°C                    17°C

IRINGA         25°C                    18°C

NJOMBE       18°C                    13°C

MWANZA     28°C                    19°C

TABORA        29°C                    18°C

TANGA          31°C                    22°C

ZANZIBAR     33°C                    26°C

........

Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 40 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki

kwa Pwani ya Kaskazini, na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.

Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa.

Matarajio kwa siku ya Jumamosi tarehe 23/01/2021: Kuendelea kwa mvua katika maeneo ya nyanda za juu Kusini

magharibi na Pwani ya Kusini.

Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 21/01/2021.

Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Post a Comment

0 Comments