Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan akifungua Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2021 lenye lengo la kutangaza fursa za Uwekezaji katika Sekta za Madini ziliopo nchini na kuwaunganisha pamoja wachimbaji na watoa huduma kwenye shughuli mbalimbali zinazofanyika migodini.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia bidhaa mbalimbali za mapambo alipotembelea maonesho ya shughuli za madini katika Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2021 lenye lengo la kutangaza fursa za uwekezaji katika Sekta za Madini ziliopo nchini na kuwaunganisha pamoja wachimbaji na watoa huduma kwenye shughuli mbalimbali zinazofanyika migodini. Kushoto ni Waziri wa Madini, Mhe. Doto Biteko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiangalia moja ya kifaa kinachotumika kwa utafiti wa kuweza kujua ubora na uhalisia wa madini XRF alipotembelea banda la Tume ya Madini kwenye maonesho ya shughuli za madini katika Kongamano la Kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2021 lenye lengo la kutangaza fursa za Uwekezaji katika Sekta za Madini ziliopo Nchini na kuwaunganisha pamoja Wachimbaji na watoa huduma kwenye Shughuli mbalimbali zinazofanyika migodini.Kushoto ni Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, akikabidhi Tuzo kwa Mwakilishi wa Kampuni ya Geita Gold Mine Tanzania, Simon Peter Shayo kwa kutambua mchango wa kampuni hiyo na kufanya vizuri katika kutekeleza sheria zinazosimamia Sekta ya Madini na Mchango wa Mlipa Kodi na Wadau walioshiriki vizuri kwa Jamii CSR hapa nchini, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2021 lenye lengo la kutangaza fursa za Uwekezaji katika Sekta za Madini ziliopo Nchini na kuwaunganisha pamoja Wachimbaji na watoa huduma kwenye Shughuli mbalimbali zinazofanyika Migodini.Kushoto ni Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akiagana na Waziri wa Madini Mhe. Doto Biteko baada ya kufungua Kongamano la kimataifa la Uwekezaji katika Sekta ya Madini 2021 lenye lengo la kutangaza fursa za Uwekezaji katika Sekta za Madini ziliopo nchini na kuwaunganisha pamoja Wachimbaji na watoa huduma kwenye Shughuli mbalimbali zinazofanyika Migodini lenye kauli mbiu “Sekta ya Madini kwa Uchumi Imara na Maendeleo Endelevu” katika Kituo cha mikutano cha Kimataifa cha Mwalimu Nyerere JNICC Jijini Dar es salaam leo Febuari 22,2021.(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais).
Kwa upande wake, Waziri wa Madini, Mheshimiwa Doto Biteko ameema, Rais Dkt. Magufuli ametoa fursa ya kuchimba madini na kufanya biashara, "tuitumie fursa hii kwa uaminifu na kuhakikisha wote tunanufaika na sekta hii, wale ambao ni wachache wanaotaka kuturudisha nyuma tutashughulika nao kwani tunatamani sekta hii iwe rafiki na ifanyike kwa uwazi ili kila aliyewekeza aione faida.
"Yapo matukio ya utoroshaji wa madini yanayoendelea nchini, nalaani matukio haya. Nawaomba wachimbaji wote tuache utoroshaji na badala yake tuangalie mbele kwa sababu hakuna kitu ambacho mchimbaji alikihitaji akakikosa.Nawaomba wanaotaka kuleta madini kutoka nchi mbalimbali kuwa tuna masoko yanayofanya biashara hiyo hivyo wafanye biashara kupitia masoko hayo na sio kukutana hotelini,"amesema Waziri Biteko.
Naye Rais na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Barrick, Dkt. Mark Bristow amesema, mwaka mmoja uliopita, Serikali ilitia saini mkataba wa kimataifa wa ushirikiano na kampuni ya Barrick ulioweza kuzaa matunda kwa Serikali ya Tanzania, jamii na wanahisa wa Barrick.
"Huu ni mfano muhimu wa kuigwa wa pande zote mbili kuweza kunufaika na tumeweza kutoa mfano barani Afrika kwa wawekezaji wote.
"Tanzania ilikuwa ni nchi ya kwanza barani Afrika kuanzisha mkataba wa kisasa wa madini hapo mwaka 1997 kwa lengo la kuvutia wawekezaji katika tasnia ya madini, Tanzania inaongoza sasa katika kutekeleza uchimbaji na uwekezaji katika madini ambao unaruhusu kuchangia manufaa yatokanayo na madini kwa kupitia ubia na ushirikishwaji wa ukweli,"amefafanua Dkt.Bristow.