Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Ajira na Mahusiano kupitia kitengo cha Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waaajiri imetoa Mafunzo kwa Viongozi na Wafanyakazi wa Vyama vya Wafanyakazi, Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) na Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) kwa lengo la kuwajengea uwezo, utawala bora na kuongeza tija miongoni mwa viongozi hao.
Akizungumza wakati akifungua mafunzo hayo yanayofanyika katika Ukumbi wa Kings Way, jana Agosti 12, 2026, mkoani Morogoro, Msajili wa Vyama vya Wafanyakazi na Waajiri, Vallensi Wambali, alipomuwakilisha Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Ajira na Mahusiano, Bi. Mary Maganga, amesema mafunzo hayo yana mchango mkubwa katika utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, inayolenga kujenga Taifa lenye rasilimali watu wenye ujuzi, taasisi zinazowajibika na mazingira bora ya kazi yanayochochea tija na maendeleo ya Nchi.
“Hatuwezi kufikia Dira 2050 bila kuwa na vyama vya wafanyakazi na waajiri vyenye nguvu, vinavyoendeshwa kwa uwazi na vinavyojenga ushirikiano badala ya migogoro,” amesema Wambali.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo
















