Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ustawi na Maendeleo ya Jamii imeishauri Serikali kuiongezea wataalam Wakala wa Usalama na Afya Mahali pa Kazi (OSHA) ili Taasisi hiyo iweze kuimarisha afya, usalama na ustawi wa wafanyakazi nchini.


Ushauri huo umetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Hawa Chakoma, Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akifungua kikao cha Kamati kilicholenga kupitia taarifa ya utekelezaji wa Sheria ya Usalama na Afya Mahali pa Kazi, Sura Namba 297, Toleo ya 2023 ikiangazia mwenendo wa usajili wa maeneo ya kazi pamoja nautoaji wa elimu ya usalama na afya mahali pa kazi kwa umma kwa mwaka wa fedha 2025/2026.








Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo




















