Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today February 15th, 2021

UTABIRI WA HALI YA HEWA KWA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3.00 USIKU WA LEO:TAREHE: 15/02/2021.

Mikoa ya Shinyanga, Simiyu, Kagera, Geita, Mara, Mwanza, Kigoma, Tabora, Katavi: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
..........
Mikoa ya Rukwa, Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe, Lindi, Mtwara Ruvuma, Dodoma, Singida pamoja na Kusini mwa mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua katika maeneo machache na vipindi vya jua.
..........
Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Manyara, Kilimanjaro, Arusha, Tanga (Visiwa vya Unguja na Pemba) pamoja na Kaskazini mwa mkoa wa Morogoro: Inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
...........
VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 24°C 16°C
D'SALAAM 32°C 25°C
DODOMA 27°C 18°C
KIGOMA 29°C 21°C
MBEYA 26°C 18°C
IRINGA 24°C 17°C
NJOMBE 21°C 12°C
MWANZA 28°C 20°C
TABORA 27°C 18°C
TANGA 32°C 24°C
ZANZIBAR 33°C 26°C
.............
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 40 kwa saa kwa Pwani yote; kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kutoka Kaskazini kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Makubwa.
Matarajio kwa siku ya Jumatano tarehe 17/02/2021: Kupungua kwa mvua katika maeneo mengi ya nchi.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 15/02/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news