Magazeti leo Juni 6,2026

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dkt. Rhimo Nyansaho, amesema kuwa sera ya ulinzi ni mhimili muhimu unaolinda usalama wa taifa na kuweka msingi imara wa maendeleo ya kijamii, kiuchumi na kisiasa, huku akisisitiza umuhimu wa kuendelea kuimarisha uwezo wa taifa wa kukabiliana na changamoto za kiusalama zinazojitokeza katika mazingira ya sasa ya dunia.
Dkt. Nyansaho ametoa kauli hiyo Aprili 4, 2026 alipowasilisha mhadhara wa kimkakati katika Chuo cha Taifa cha Ulinzi Tanzania (National Defence College – Tanzania) kilichopo Kunduchi, Dar es Salaam, kwa washiriki wa Kozi ya Kistrategia ya 14, chini ya mada “Umuhimu wa Sera ya Ulinzi katika Kuimarisha Usalama wa Taifa.”

Katika mhadhara wake, Waziri Nyansaho ameeleza kuwa sera ya ulinzi si nyaraka za kawaida za serikali bali ni dira inayotoa mwongozo wa kimkakati katika kulinda mipaka, watu na rasilimali za taifa, huku ikihakikisha nchi inakuwa salama na yenye utulivu wa kutosha kuendeleza shughuli za maendeleo.

“Usalama wa taifa ni msingi wa maendeleo. Bila usalama, ustawi wa uchumi, uwekezaji na huduma za kijamii haviwezi kufikiwa kwa ufanisi unaotarajiwa,” amesisitiza Waziri Nyansaho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here