Utabiri wa hali ya hewa/ Weather Forecast today February 25th, 2021

UTABIRI WA HALI YA HEWA WA SAA 24 ZIJAZO KUANZIA SAA 3 USIKU WA LEO TAREHE 25/02/2021

Mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Rukwa, Njombe, Ruvuma, Kusini mwa Mkoa wa Morogoro, Kagera, Geita, Mwanza, Shinyanga, Kigoma, Tabora, Katavi, Lindi na Mtwara inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, mvua na ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
............
Mikoa ya Mara na Simiyu inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, ngurumo katika maeneo machache na vipindi vya jua.
............
Mikoa ya Pwani (ikijumuisha Visiwa vya Mafia), Kaskazini mwa Mkoa wa Morogoro, Dar es Salaam, Tanga, Dodoma, Singida
Visiwa vya Unguja na Pemba inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi, Mvua nyepesi katika maeneo machache na vipindi vya jua.
............
Mikoa ya Manyara, Kilimanjaro na Arusha inatarajiwa kuwa na Hali ya mawingu kiasi na vipindi vya jua.
............
VIWANGO VYA JOTO, VYA JUA KWA BAADHI YA MIJI HAPA NCHINI:
MJI Kiwango cha juu Kiwango cha chini
cha joto cha joto
ARUSHA 28°C 18°C
D'SALAAM 31°C 25°C
DODOMA 26°C 19°C
KIGOMA 28°C 17°C
MBEYA 25°C 14°C
IRINGA 26°C 16°C
NJOMBE 19°C 12°C
MWANZA 25°C 22°C
TABORA 27°C 18°C
TANGA 33°C 25°C
ZANZIBAR 32°C 25°C
.......................
Upepo wa Pwani: Unatarajiwa kuvuma kwa kasi ya km 20 kwa saa kutoka Kaskazini Mashariki kwa Pwani ya Kaskazini na kwa kasi ya km 30 kwa saa kutoka Kaskazini Magharibi kwa Pwani ya Kusini.
Hali ya Bahari: Inatarajiwa kuwa na Mawimbi Madogo.
Matarajio kwa siku ya Jumamosi tarehe 27/02/2021: Mabadiliko Kidogo.
Utabiri huu umetolewa leo tarehe: 25/02/2021.
Na: MAMLAKA YA HALI YA HEWA TANZANIA.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news