Namungo FC yatinga hatua ya makundi Kombe la Shirikisho Afrika,Clube Desportivo 1º de Agosto yachapwa 7-5

Namungo FC leo Februari 25, 2021 imefanikiwa kutinga katika hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika, licha ya kupokea kipigo cha mabao 3-1 kutoka kwa Clube Desportivo 1º de Agosto ya Angola, anaripoti Mwandishi Diramakini.
Ni kupitia mtanange uliopigwa katika dimba la Azam Complex lililopo katika Halmashauri ya Wilaya ya Temeke mkoani Dar es Salaam leo Februari 25, 2021.

Namungo wamefanikiwa kutinga hatua hiyo kwa matokeo ya jumla ya ushindi wa mabao 7-5, kufuatia ushindi wa mabao 6-2 walioupata Namungo katika mchezo wa kwanza uliopigwa Februari 21, mwaka huu.

Katika hatua hiyo, Namungo imepangwa Kundi D ikiwa na Raja Casablanca ya Morocco, Pyramids FC ya Misri na Nkana FC ya Zambia.

Hii ni hatua ya kipekee kwa timu hiyo kutoka mkoani Lindi ikiwa ni mara yake ya kwanza kushiriki michuano ya Kimataifa na kufikia hatua hii.

Post a Comment

0 Comments