Mwanza kunufaika na Kiwanda cha kusafisha Dhahabu

Kukamilika kwa Ujenzi wa Kiwanda cha Kusafisha Madini ya Dhahabu kwa kiwango kikubwa barani Afrika cha Mwanza Precious Metals Refinery Ltd kinatarajiwa kuleta mapinduzi makubwa ya kiuchumi Mkoani humo na Taifa, hususan kupitia biashara ya madini, anaripoti Asteria Muhozya (WM) Dodoma.
Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Seif Gulamali (mbele) akizungumza jambo wakati wa kikao cha Kamati hiyo na Viongozi na Watendaji wa Wizara ya Madini na Taasisi zake. Kulia kwake ni Katibu wa Kamati Danford Mpelumbe. Wengine wanaofuatilia ni wajumbe wa Kamati hiyo.
Aidha, Kiwanda hicho kinachotajwa kuwa na teknolojia ya kisasa ya kusafisha dhahabu mpaka 999.9 purity kinapelekea dhahabu kutoka Tanzania kuwa na ubora wa kimataifa wa kununuliwa na Benki Kuu duniani kwa ajli ya kuhifadhiwa.

Hayo yamebainishwa leo Machi 10, na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse wakati akitoa taarifa kuhusu utekelezaji wa mradi wa kiwanda hicho kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, jijini Dodoma.
Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini wakifuatilia Taarifa zilizowasilishwa na Wizara ya Madini na Taasisi zake kwa Kamati hiyo.

Dkt. Mwasse ameongeza kuwa, kiwanda hicho kimewekewa uwezekano wa kuongeza uzalishaji wa hadi kilo 960 kwa siku tofauti na kilo 480 kwa siku ambazo zimepangwa kusafishwa mara baada ya kuanza kazi mwishoni mwa mwezi Machi, 2021.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Madini, Prof. Simon Msanjila akiwasilisha kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini Taarifa kuhusu Mradi wa Kituo cha Mfano kwa Wachimbaji Wadogo cha Katente- Chunya pamoja na Taarifa kuhusu Eneo Tengefu la Mirerani.

Pia, Dkt. Venance amesema kuwa, ujenzi wa kiwanda hicho ambacho ni kikubwa kwa usafishaji dhahabu, ikilinganishwa na mitambo ya nchi za Afrika ya Kusini na Sudan ni matokeo ya Marekebisho ya Sheria ya Madini ya Mwaka 2017 ambayo yalichangiwa na kutungwa kwa Sheria ya Natural Wealth and Resources (Permanent sovereghty ya mwaka 2017, ambayo iliweka msisitizo kuhusuiana na rasilimali za nchi na matakwa ya nchi kufaidika na madini yanayochimbwa nchini kwa kuyaongezea thamani kabla ya kusafirishwa nje ya nchi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Madini (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse akiwasilisha taarifa kuhusu Mradi wa Kusafisha Dhahabu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Akizugumzia vyanzo vya malighafi katika kiwanda hicho amesema, vitatoka kwa wachimbaji wadogo kupitia mradi wa kusaidia wachimbaji wadogo (ASM Support project), wachimbaji wakubwa wenye migodi hapa nchini, dhahabu kutoka nchi jirani na dhahabu kutoka kwa madalali.

Akifafanua kuhusu faida za ujenzi wa kiwanda hicho amesema kuwa ni pamoja na kuongeza mapato kwa nchi kupitia mrabaha na ada za ukaguzi, kuongeza mapato ya Halmashauri kilipo kiwanda hicho kupitia ushuru wa huduma, kuongeza ajira kwa taifa ambapo mradi unatarajia kuajiri watumishi 120 wengi wakiwa watanzania na wachache kutoka nje ya nchi ikihusisha ajira za wakandarasi, wazalishaji wa dhahabu, wazabuni, watoa huduma na wasafirishaji.

Vilevile, amezitaja faida nyingine za ujenzi wa kiwanda hicho kuwa ni pamoja na kuwezesh Benki Kuu kuanza kununua dhdhabu kwa mujibu wa sheria za nchi, serikali kuanza kukusanya mrabaha kwa kuchukua dhahabu badala ya fedha, dhahabu inayozalishwa Tanzania kuanza kutambulika na kuwa na nembo yake maluum, kuwa na kituo cha kuuza tofari za dhdhabu kutoka kwa wazalishajimbalimbali wa dhahabu ndani na nje ya nchi na huduma wa jamii inayozunguka mradi huo.

Mradi wa Mwanza Precious Metals Refinery ni Ubia kati ya STAMICO, kampuni ya Rozelia General Trading LLC ya Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) pamoja na Kampui ya ACME Consultant Engineers PTE Ltd ya Singapore. STAMICO inamiliki asilimia 25 na wabia asilimia 75.
Makamu Mwenyekiti wa Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini, Seif Gulamali, akifuatilia taarifa kuhusu Kiwanda cha Kusafisha Dhahabu cha Mwanza iliyotolewa na Kaimu Mtendaji wa Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) Dkt. Venance Mwasse. Wengine wanafuatilia ni wajumbe wa kamati husika.

Aidha, kulingana na taarifa ya Dkt. Mwasse kwa Kamati, amesema hisa za STAMICO zitakuwa zikiongezeka kwa asilimia 5 kwa kipindi cha miaka 15 na hivyo kuifanya STAMICO kumiliki asilimia 51 na wabia asilimia 49.
Vilevile Dkt. Mwasse amesema STAMICO itakuwa inapata asilimia 2.5 ya mauzo ghafi kama ada ya huduma za usimamizi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news