🔴𝐋𝐈𝐕𝐄:MWADUI FC VS SIMBA SC MTANANGE WA LIGI KUU TANZANIA BARA (VPL)

Nahodha John Raphael Bocco leo ameipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara Uwanja wa Kambarage mjini Shinyanga. 

Bocco amefunga bao hilo dakika ya 66 kwa kichwa akimalizia mpira uliounganishwa kwa kichwa pia na beki Mkenya, Joash Onyango kufuatia kona ya winga Mghana, Bernard Morrison kutoka upande wa kulia.

Ushindi huo unawafanya Wekundu hao wa Msimbazi wafikishe pointi 52 baada ya kucheza mechi 22 na kurejea nafasi ya pili, sasa wakizidiwa pointi mbili na Yanga SC ambao hata hivyo wamecheza mechi tatu zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news