Serengeti Breweries Limited yaja na Programu ya Kilimo-Viwanda

Kampuni ya bia ya Serengeti Breweries Limited (SBL) imejidhatiti kuwapa wanafunzi nyenzo na mafunzo zaidi ya kivitendo kama njia mojawapo ya kuongeza idadi ya wataalamu wa kilimo nchini Tanzania, ANARIPOTI MWANDISHI DIRAMAKINI.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries Mark Ocitti, akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza, wakati wanafunzi ambao ni wa nufaika wa programu ya Kilimo-Viwanda kutoka chuo cha kilimo cha Igabiro wilayani Muleba mkoani Kagera walipotembelea kiwanda cha Mwanza kujionea uzalishaji wa bia, kulia ni Mkuu wa chuo hicho Sadock Stefano.

Hayo yamesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SBL, Mark Ocitti katika tukio la kuwapongeza wananfunzi 17 waliopata nafasi za ufadhili kupitia programu hii kutoka chuo cha Igabiro Training Institute of Agriculture kilichopo mkoa wa Kagera. SBL imelenga kufanya haya kupitia program hii maarufu inayojulikana kama Kilimo Viwanda inayolenga kusaidia wanafunzi kutoka familia masikini ili waweze kusomea masomo ya kilimo kwenye ngazi ya diploma katika vyuo vya ndani.

Ocitti alisema, “Programu ya Kilimo-Viwanda inawajengea wanafunzi uwezo wa kuelewa kimatendo, ambao ni mfumo nje ya mafunzo yao ya kila siku darasani, mfano kutembelea viwanda vyetu vya bia na mashambani’’. Ocitti alifafanua kuwa ufadhili huu unajumuisha malipo yote ya chuo na gharama zingine katika kipindi chao chote cha masomo.
Mwanafunzi wa chuo cha Kilimo lgabiro cha mkoani Kagera Neema Michael, akizungumza jinsi alivyonuifa kwa kulipiwa ada na kampuni ya Serengeti Breweries kupitia programu ya Kilimo-Viwanda, ambapo wanafunzi wa chuo hicho walitbelea kiwanda cha Mwanza. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa SBL Mark Ocitti na anayefuatia na mkuu wa chuo hicho , Sadock Stephano.

Halikadhalika, Ocitti alisema kuwa, programu hii imedhamiria kuongeza nguvu juhudi za serikali katika kuongeza wataalamu zaidi wa kilimo nchini. SBL inafanya kazi na mtandao wa wakulima 400 kwenye mikoa nane nchini ambapo wananunua nafaka kwa ajili ya uzalishaji bia. SBL inatumia takribani tani 17,000 sawasawa na asilimia 70 na mahitaji yao kwa mwaka.
Wanafunzi wa chuo cha Kilimo Igabiro kilichopo Muleba mkoani Kagera ambao ni wanufaika wa programu ya ufadhili wa mosomo ya Kampuni ya Bia ya Serengeti inayojulikana kama Kilimo Viwanda wakiwa lkatika ziara ya kutembelea kiwanda cha kilichopo Mwanza.
Mpishi wa bia wa zamu(Shift Brewer) Christina Machaka akiwaeleza namna bia inavyopikwa kwenye mitungi maalum wanafunzi wa chuo cha kilimo lgabiro walipotembelea kiwanda cha bia cha Serengeti tawi la Mwanza, walipotembelea kiwanda hicho ikiwa ni sehemu ya kujifunza kwa vitendo kupitia wa programu ya Kilimo-Viwanda inayoendeshwa na kampuni ya Serengeti.

Programu hii iliyoanzishwa mwaka 2020 imesaidia wanafunzi 70 kusomea kozi za diploma katika ujuzi wa kilimo katika vyuo vingine vitatu ambavyo ni Kaole Wazazi College of Agriculture (Bagamoyo), Kilacha Agriculture Training Institute (Moshi) na St. Maria Goretti Agriculture Training Institute (Iringa).

Katika upande wake Mkuu wa Chuo cha Igabiro Training Insitute of Agriculture, Sadock Stephano, aliipongeza SBL kwa msaada wao wa dhati na kusisitza makampuni mengine waige mfano katika kuwasaidia wanafunzi kutoka familia masikini nchini

Post a Comment

0 Comments