Simba SC yalia na TFF, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara


Taarifa kutoka idara ya habari ya klabu ya Simba kuhusu sakata la kuahirishwa kwa mchezo wao wa jana dhidi ya Yanga.

>Simba wanadai walipigiwa simu na TFF pamoja na bodi ya Ligi saa 7 mchana na baadae wakatumiwa barua rasmi.

> TFF na Bodi ya Ligi waliwaambia Simba kuwa wameshawasiliana na Yanga kuhusu kusogezwa mbele kwa muda wa kuanza mchezo na Yanga wamekubali.

> Idara ya habari ya Simba inadai kosa alilofanya Yanga linapaswa kuchukuliwa hatua ya kushushwa madaraja mawili na Simba kupewa alama 3 na magoli mawili kwa mujibu wa kanuni.

Post a Comment

0 Comments