Timu ya Usimamizi wa Huduma ya Afya OR-TAMISEMI yafanya ziara Singida

Timu ya Usimamizi wa Huduma ya Afya , Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) imefanya ziara ya kikazi katika Mkoa wa Singida, ANARIPOTI MWANDISHI DIRAMAKINI.
Ziara hiyo imefanyika Mei 6, mwaka huu ambapo timu hiyo ilifanya kikao kazi na timu za uendeshaji na usimamizi wa huduma za afya Mkoa na Halmashauri za Mkoa wa Singida.

Lengo likiwa ni kuangalia utoaji wa huduma bora za afya, matumizi ya fedha na uimarishaji wa ukusanyaji wa Bima ya Afya ya CHF ya papo kwa papo, tiba na vitendanishi, maendeleo ya miradi na kujua changamoto za utumishi.
Akizungumza kuhusu masuala ya kiutumishi, Afisa Utumishi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Bi. Joyce Mushi amezishauri timu hizo kuhakikisha wanaandaa na kutoa mafunzo ya awali kwa watumishi wapya wanaopangiwa kazi katika halmashauri zao ili kuwajengea uwezo na uelewa wa mazingira ya kazi, Sheria , Kanuni na Taratibu za Utumishi wa Umma.

Mkoa wa Singida una jumla ya vituo 245 vya kutolea huduma za afya, ikiwa ni hospitali 11, vituo vya afya 20 na zahanati 210.

Post a Comment

0 Comments