Mbowe aongoza viongozi wa CHADEMA Taifa maziko ya Profesa Baregu leo


Na Mwandishi Diramakini

Mwenyekiti wa Chadema Taifa Mhe. Freeman Mbowe na Katibu Mkuu wa Chadema Mhe. John Mnyika Juni 19, 2021 akiwa na viongozi wengine wamewasili mkoani Kagera tayari kushiriki maziko ya Profesa Mwesiga Baregu, aliyekuwa mjumbe wa Kamati Kuu ya chama leo Juni 20, 2021.
Awali katika Mkoa wa Dar es Salaam mamia ya wananchi wakiwemo wanazuoni na viongozi wa vyama vya siasa walishiriki ibada ya kumuaga msomi, mwanasiasa na kada wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Profesa Mwesiga Baregu.

Ibada ya kumuaga Profesa Baregu ambaye amewahi kuwa mjumbe wa kamati kuu ya Chadema ilifanyika Juni 18, 2021 katika Kanisa ka Kiinjili la Kilutheri Tanzania Kunduchi, Dar es Salaam.

Viongozi wa vyama ya siasa waliohudhuria ni mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe; mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba; mwenyekiti wa UDP, John Cheyo na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamdu Shaka.

Mara baada ya ibada kumalizika, mwili wa msomi huyo unapelekwa Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kusafirishwa kuelekea Bukoba mkoani Kagera kwa maziko yatakayofanyika leo.

Profesa Baregu alifariki dunia Juni 13, 2021 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alikokuwa akipatiwa matibabu.

Post a Comment

0 Comments