Rais Samia atengua uteuzi wa DC Msulwa, DED Sheilla Lukuba

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 15 Juni, 2021 ametengua uteuzi wa Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Bw. Bakari Msulwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Wilaya hiyo, Bi. Sheilla Lukuba kwa kushindwa kusimamia Wafanyabishara wadogo wadogo (Wamachinga) mkoani Morogoro.

Mhe. Rais Samia ametangaza hatua hiyo wakati akihutubia vijana wa Mkoa wa Mwanza na mikoa jirani waliowawakilisha vijana wote nchini.

Amesema, amesikitishwa na kitendo cha Asakri Mgambo katika eneo la Kituo cha Mabasi Morogoro kuwanyanyasa Wafanyabishara wadogo maarufu kama Wamachinga wanaofanya baishara nje ya Kituo hicho.

Mhe. Rais amesema kitendo cha kunyanyaswa wafanyabishara hao si cha kiungwana na hakikubali kamwe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

Post a Comment

0 Comments