Afrika yaonyesha matumaini michezo ya Olimpiki mjini Tokyo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI
 
Bara la Afrika limepata ushindi wa awali katika mashindano ya ndondi ya Olimpiki yanayoendelea mjini Tokyo nchini Japan wakati michezo ikiingia wiki yake ya kwanza.

Ushindi ho wa Julai 26, 2021 pia ulikuwa si wa furaha sana baada ya mwanamke pekee kutoka Somalia kutolewa kwenye mashindano hayo.

Ramla Said Ahmed Ali alipoteza pambano lake la uzani wa Feather kwa pointi 5-0 dhidi ya Maria Claudia Nechita wa Romania.

Ni wakati bondia mwingine wa kike Khouloud Moulahi Hlimi wa Tunisia akipoteza pia kwa pointi 5-0 dhidi ya Sena Irie wa Japan pia katika uzani wa Feather.

Kwa upande wa wanaume Tetteh Sulemanu wa Ghana alifuzu kuingia raundi inayofuata baada ya kumshinda Rodrigo de la Rosa Marte wa Jamhuri ya Dominican 3-2 kwa uzani wa Fly, wakati Patrick Chinyemba wa Zambia alimshinda Alex Winwood wa Australia 4-1 pia katika uzani huo huo wa Fly.

Naye Younes Nemouchi wa Algeria alimshinda David Kavuma Ssemujju wa Uganda katika uzani wa kati wakati David Mwenekabwe Tshama wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo akimshinda Dieudonne Ntsengue Seyi wa Cameroon 3-2 pia katika uzani huo wa kati.

Hata hivyo,Rajab Otukile Mohammed wa Botswana alishindwa na Martinez Rivas wa Colombia katika uzani wa Fly.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news