Tume ya Ushindani (FCC) imesema itaendelea kusimamia kwa karibu haki za walaji kwa taasisi na kampuni zinazotumia mikataba iliyoandaliwa kwa upande mmoja, ili kuhakikisha watumiaji wa huduma na bidhaa hawapati hasara kutokana na mikataba hiyo.

Kauli hiyo imetolewa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa FCC, Khadija Ngasongwa, alipokuwa akizungumza katika semina ya wadau kutoka taasisi na kampuni zinazotumia mikataba ya upande mmoja, iliyofanyika jijini Dar es Salaam.
Ngasongwa alisema FCC inaendelea kufuatilia kwa karibu mikataba ya aina hiyo ili kuhakikisha haikiuki haki za walaji katika soko. Alifafanua kuwa mikataba ya upande mmoja hutumiwa sana na taasisi mbalimbali kwa lengo la kurahisisha utoaji wa huduma kwa wakati, lakini ni muhimu iwe chini ya uangalizi ili kuepuka matumizi yanayoweza kuwa kinyume na sheria za ushindani na ulinzi wa mlaji.
Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo

































