Mbunge Jerry Silaa: Wabunge waanze kulipa kodi "Vikiliwa vya Mwali na vya Kungwi viliwe"

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mbunge wa Ukonga katika Jiji la Ilala mkoani Dar es Salaam, Mheshimiwa Jerry Silaa amesema imefikia hatua wabunge waanze kulipa kodi.

Ni kupitia mishahara yao ili wapate uwezo wa kuwaambia wananchi na wao walipe kodi.
Mheshimiwa Silaa ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliowashirikisha wananchi wa Mzinga Ukonga mkoani Dar es Salaam wakati akizungumzia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo jimboni kwake.

"Mie nimeanza Ubunge juzi mwaka jana mwezi wa 11, kwa hiyo nimekuta hayo yanayosemwa mengine yameshapitishwa tayari Bungeni na katika hili niungane na Mbunge wa Kinondoni, Abbas Tarimba kwamba vikiliwa vya Mwali na vya Kungwi viliwe.
Ni wakati muafaka sisi waheshimiwa wabunge ili tupate uwezo wa kuwaambia watu waanze kulipa kodi na sisi tuanze kulipa kodi katika mishahara yetu, hakuna sababu ya kuwa wengine wanalipa, wengine hawalipi ukishakuwa haulipi unakosa ile nguvu ya kumwambia mwenzako alipe.

“Kwa hiyo niseme tu kwamba kazi kubwa inayotakiwa tuifanye sisi kama viongozi ni kutowadanganya Watanzania kwamba tunaweza kuiendesha nchi bila kodi, haitowezekana,"amesema.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news