Magazeti leo Juni 5,2026

Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimesisitiza umuhimu wa kuwekeza katika tafiti, ubunifu na teknolojia za uzalishaji wa mbegu bora ili kuongeza tija katika sekta ya kilimo na kuimarisha usalama wa chakula nchini.
Kauli hiyo imetolewa wakati wa mjadala wa masuala ya uwekezaji katika miradi ya maendeleo ya uzalishaji wa mbegu na ubunifu wa teknolojia za kilimo ulioandaliwa na SUA kwa kushirikisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo, wakiwemo watafiti, taasisi za kifedha, wazalishaji wa mbegu na Taasisi ya Kudhibiti Ubora wa Mbegu Tanzania (TOSCI).

Akizungumza kwa niaba ya Makamu Mkuu wa SUA, Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Taaluma, Utafiti na Ushauri wa Kitaalam, Prof. Maulid Mwatawala, alisema maendeleo ya sekta ya kilimo yanategemea kwa kiwango kikubwa uwekezaji katika teknolojia rahisi, tafiti na ubunifu unaolenga kutatua changamoto zinazowakabili wakulima.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

Know matter how large or small your business is, advertising here