Aliyemuua mke wake kwa kipigo kisa wivu wa mapenzi ajinyonga

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Lucas Mangu mwenye umri wa miaka 46 amefariki dunia kwa kujinyonga mara baada ya kumuua mke wake,Anna Kisino (41).
Mkazi huyo wa Mtaa wa Kiongozi uliopo mjini Babati Mkoa wa Manyara anadaiwa kuchukua uamuzi huo baada ya kumpiga na kumsababishia kifo mke wake kutokana na wivu wa mapenzi.

Hayo yamebainishwa leo Agosti 23, 2021 na Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Marrison Mwakyoma wakati akizungumzia tukio hilo.

Kamanda huyo amesema, tukio hilo limetokea usiku wa Agosti 22, 2021 mjini hapa ambapo Lukas Mangu alimuua mkewe kwa kumpiga sehemu mbalimbali za mwili hadi kumuua baada ya kumfungia ndani kutokana na wivu.

Pia amesema, Lukas Mangu alikuwa amesafiri kwenda Wilaya ya Mvomero Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya shughuli za kilimo na alirudi Babati siku hiyo na kufanya mauaji hayo ya mkewe na kujiua.

Kamanda Mwakyoma amesema, siku hiyo baada ya kurudi nyumbani ghafla bila taarifa alimkosa nyumbani mke wake ambaye alitoka kidogo na aliporudi akamuuliza alikuwa wapi na kuanza kumpiga.

Amesema, watu walijaribu kusuluhisha ili aache kumpiga mkewe baada ya kusikia yowe ila kwa kuwa alifunga mlango akimpiga aliwaambia wamuache ampige kwani ni mke wake.


MUHIMU


UNATAMANI DIRAMAKINI BLOG TUWE HEWANI SAA 24 KUKUPA HABARI ZA KINA KILA DAKIKA, TUNAOMBA UTUUNGE MKONO KWA KUCHANGIA GHARAMA ZA MAWASILIANO NA INTANETI KWA WAANDISHI WETU POPOTE WALIPO NDANI NA NJE YA TANZANIA; TUNAPOKEA MCHANGO WAKO KUPITIA 0719254464 (Tigo Pesa-Godfrey Nnko) AU UKIHITAJI NAMBA YA BENKI TUJULISHE. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA SAPOTI YAKO. ASANTE

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news