MAKAMBA ACHANGIA MILIONII 5/- SHULE YA SEKONDARI JANUARY MAKAMBA

Na Yusuph Mussa, Bumbuli

MBUNGE wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga January Makamba ametoa fedha taslimu sh. milioni tano kwa Shule ya Sekondari January Makamba ili waweze kununua madawati.
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga January Makamba (kushoto) akiweka jiwe la msingi ujenzi wa maabara Shule ya Sekondari January Makamba iliyopo Kata ya Kwemkomole katika Halmashauri ya Bumbuli. Kulia ni Diwani wa Kata ya Kwemkomole Hozza Mandia (Picha na Yusuph Mussa).

Shule hiyo iliyopo Kata ya Kwemkomole, Tarafa ya Mgwashi katika Halmashauri ya Bumbuli inakabiliwa na upungufu wa madawati 146, huku yaliyopo yakiwa 180, hivyo kufanya hiyo yenye wanafunzi 326 baadhi yao kukosa madawati ya kukalia.

Makamba alitoa fedha hizo hivi karibuni alipofika kukagua miradi ya maendeleo, huku akiahidi kupunguza changamoto moja baada ya nyingine kwenye shule hiyo ili iendane na jina lake ambalo iliitwa January Makamba kwa matakwa ya wananchi, baada ya kuona mchango wake ni mkubwa kwenye shule hiyo.

"Nitajaribu kupunguza changamoto za shule hii moja baada ya nyingine ili iweze kufanana na jina lake. Ni kweli mna tatizo la maabara, ambayo bado ni boma, na inatakiwa kumaliziwa. Lakini pia kunatakiwa kuwa na maktaba, chumba cha kompyuta na fursa nyingine. Kwa sasa mmepata walimu wa sayansi, hivyo haiwezekani mkose maabara au chumba cha kompyuta kwa ajili ya kujifunza.
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga January Makamba (wa pili kulia) akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa wananchi wa Kata ya Kwemkomole. Walimpa zawafi hiyo alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo, na kufika Shule ya Sekondari ya kata hiyo ambayo waliipa jina la January Makamba. Na mbuzi huyo ni ishara ya kuthamini mchango wake. Kulia ni Diwani wa Kata ya Kwemkomole ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli, Hozza Mandia (Picha na Yusuph Mussa).
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga January Makamba (kushoto) akipima mtambaa panya (linta) katika Zahanati ya Kijiji cha Msambya iliyopp Kata ya Kwemkomole. Ni baada ya kuhoji jengo hilo kuwa fupi. Hata hivyo alifahamishwa kuwa kuna udongo uliingia kwenye jengo hilo wakati wa mvua ndiyo maana linaonekana fupi, lakini kama litachimbwa litarudi kwenye kiwango chake. (Picha na Yusuph Mussa).
Ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kwemsambya, Kata ya Kwemkomole ukiendelea. Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga January Makamba alifika juzi kuangalia ujenzi huo. (Picha na Yusuph Mussa).
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga January Makamba (kulia) akimkabidhi fedha taslimu sh. milioni moja Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Kwemsambya, Kata ya Kwemkomole Husna Ramadhan (kushoto) kwa ajili ya ukarabati wa vyumba vya madarasa Shule ya Msingi Kwemsambya. (Picha na Yusuph Mussa).
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli mkoani Tanga January Makamba (wa pili kulia) akipokea zawadi ya mbuzi kutoka kwa wananchi wa Kijiji cha Kwemsambya, Kata ya Kwemkomole. Walimpa zawafi hiyo alipofanya ziara ya kukagua miradi ya maendeleo ikiwemo zahanati ya kijiji hicho. Na mbuzi huyo ni ishara ya kuthamini mchango wake. Kulia ni Diwani wa Kata ya Kwemkomole ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Bumbuli, Hozza Mandia (Picha na Yusuph Mussa).

"Nataka kuwatia moyo, kuja kusoma shule hii hamkukosea. Akili za mtu hazijapendelewa, bali ni namna unajituma kusoma, na fursa zinazokuzunguka. Mtu yeyote miongoni mwenu, anaweza kuwa yeyote kwenye nchi hii, iwe Mbunge, Mkuu wa Wilaya, Injinia, Waziri ama Rais," alisema Makamba wakati anazungumza na wanafunzi wa shule hiyo.

Makamba aliweka jiwe la msingi la maabara hiyo ambayo, pamoja na kuichangia ujenzi wake hadi boma kukamilika huku akishirikiana na wananchi, pia ametoa bati 86 zenye thamani ya sh. milioni 2,537,000 kwa ajili ya kuezeka maabara hiyo.

Akiwa Kijiji cha Kwemsambia, Kata ya Kwemkomole, Makamba alitoa fedha taslimu sh. milioni 1,580,000, ambapo sh. milioni moja ni ukarabati wa vyumba vitano vya madarasa kati ya sita vya Shule ya Msingi Kwemsambia kwa ajili ya ukarabati kwa kuweka sakafu, na sh. 580,000 ni kununua nondo kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Kwemsambia. Kabla ya hapo, Makamba alitoa sh. milioni 1.7 kupitia Mfuko wa Jimbo kwenye zahanati hiyo ili kununua nondo, kumlipa fundi na kusafirisha nondo hizo, ambapo zahanati ipo usawa wa linta.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news