Mchungaji wa Kanisa la Sayuni akutwa amekufa baada ya kuomba azikwe akiwa hai ili afufuke kama Yesu Kristo

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mchungaji wa Kanisa la Zion (Sayuni) lililopo mjini Chidiza nchini Zambia,James Sakara amekutwa amekufa baada ya kuomba azikwe akiwa hai kaburini ili aweze kufufuka baada ya siku tatu kama Yesu Kristo.
Shuhuda mmoja mjini Chidiza ameieleza DIRAMAKINI BLOG kuwa,Mchungaji Sakara ambaye alikuwa mwenye umri wa miaka 22 alikuwa anajiamini kupita kiasi katika uwezo wake wa kuiga ufufuo wa Yesu Kristo.

"Hivyo kwake, haikuwa jambo la kupuuza wito huo kwa waumini wake, maana tayari alishajijengea mazingira makubwa ya imani baina yake na waumini na hata yeye mwenyewe,"amesema Daudi Chawezi mkazi wa mjini hapa katika mahojiano na DIRAMAKINI BLOG.

Amesema, nguvu aliyokuwa nayo ya ushawishi, Mchungaji Sakara ndiyo iliweza kuliingia kusanyiko la waumini wake na kuamini kuwa, angeweza kufufuka siku ya tatu kama Mwana wa Mungu miaka elfu kadhaa iliyopita.

DIRAMAKINI BLOG imeelezwa kuwa, Mchungaji Sakara alipata waumini watatu wa kanisa lake ambao walimsaidia kuchimba kaburi lenye kina kirefu, kufunga mikono yake na kumzika akiwa hai.

"Ni jambo la kushtua sana, kwani badala ya kufufuka baada ya siku tatu, Mchungaji Sakara alikutwa amekufa na washiriki wa Kanisa la Sayuni waliotamani kuona kiongozi wao anatimiza ahadi yake ya kufufuka ndani ya siku tatu,"ameongeza.

Hata hivyo, baada ya kuona mwili wa kiongozi wao ambaye amekufa haufufuki,waumini wengine wa kanisa walijaribu mfululizo wa mazoezi ya kiroho ili kumfufua, lakini haikufanikiwa hadi sasa.

Ingawa, baadhi ya waumini wa Sakara walipuuza maono hayo ya Mchungaji wao, walikwamishwa na nguvu kubwa ya viongozi wa juu kanisani ambao walisisitiza lazima ahadi hiyo itimizwe. Mamlaka nchini Zambia zinaendelea kufuatilia kwa karibu huku uchunguzi ukiendelea kufanyika kwa ajili ya kuwatia hatiani wote walioshiriki katika kifo hicho.

James Sakara anaondoka duniani akiwa amemuacha mke wake akiwa mjamzito na waumini ambao hawajui hatiama yao iwapo mamlaka zitaanza kupita nyumba baada ya nyumba ili kufanya uchunguzi. Pengine imani potofu kutoka kwa Mchungaji huyo zinaweza kuingia katika rekodi za baadhi ya watumishi wa Mungu barani Afrika ambao wamekuwa wakimchezea Mungu kupitia makanisa.

Ni hivi karibuni tu walijitokeza baadhi ya wachungaji wenye vituko vingi wakiwemo waliodai kuwa wana namba ya simu ya Mungu ambayo wakipiga inaweza kuwaponya maelfu ya watu aina zote za magojwa na mateso.

Miongoni mwao ni Mchungaji wa Zimbabwe, Paul Sanyangore (32) ambaye alidai kuwa na namba ya Mungu na anaweza kumpigia simu haraka na kuzungumza naye mbele ya mkutano wake muda wowote.

"Nina kituo cha moja kwa moja na Mungu, kwa kweli nina namba yake na ninaweza kumpigia wakati mahitaji yanapotokea,"alinukuliwa hivi karibuni akieleza katika moja ya mahubiri yake.

MUHIMU

UNATAMANI DIRAMAKINI BLOG TUWE HEWANI SAA 24 KUKUPA HABARI ZA KINA KILA DAKIKA, TUNAOMBA UTUUNGE MKONO KWA KUCHANGIA GHARAMA ZA MAWASILIANO NA INTANETI KWA WAANDISHI WETU POPOTE WALIPO NDANI NA NJE YA TANZANIA; TUNAPOKEA MCHANGO WAKO KUPITIA 0719254464 (Tigo Pesa-Godfrey Nnko) AU UKIHITAJI NAMBA YA BENKI TUJULISHE. MUNGU AKUBARIKI SANA KWA SAPOTI YAKO. ASANTE

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news