Mtanzania aliyetabiri ushindi wa upinzani Zambia, Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba apokelewa kwa shangwe jijini Lusaka

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa wa Kanisa la Penuel Healing Ministry la Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam, Alphonce Temba amepokelewa nchini Zambia kwa shangwe baada ya utabiri wake kuhusu ushindi wa Chama cha Upinzani cha United Party for National Development (UPND) kushinda urais kutimia.

Temba amepokelewa rasmi mjini Lusaka na uongozi wa chama hicho ili azidi kuachilia neno la ushindi na mafanikio mapya kwa uchumi wa Zambia chini ya uongozi mpya.
Amekaribishwa na mwenyeji wake mwenyekiti wa taifa wa chama tawala kilichoshinda uchaguzi nchini Zambia, Stephen Katuka jijini Lusaka leo Agosti 21,2021

Mwinjilisti Temba alitabiri juu ya ushindi wa Chama cha United Party for National Development (UPND) kilichomwingiza madarakani rais mteule, Hakainde Hichilema.

Hichilema anatarajia kuapishwa Agosti 24,2021 jijini Lusaka nchini Zambia.

Hakainde Hichilema ambaye ni mfanyabiashara na mwanasiasa wa Zambia anakuwa Rais mteule baada ya kuisaka nafasi hiyo kwa vipindi vitano bila mafanikio.

Rais huyo mteule mwaka 2006, 2008, 2011, 2015 na 2016 aligombea na kuambulia patupu, lakini ndoto yake imekuwa kweli uchaguzi wa 2021baada ya Mwinjilisti Temba kutamka neno la baraka kulingana na maono aliyopewa na Mungu.

Ushindi ambao ulitokana na kura 2,810,777 na Mheshimiwa Edgar Lungu kura 1,814,201.

"Mwinjilisti Temba siyo wa kawaida amekuwa na uwezo mkubwa sana kuwatabiria viongozi mbalimbali Afrika na kushinda nafasi za Urais hila amekuwa na tabia yake ya unyenyekevu na kujishusha iliyomchukulia watu kumuona wa kawaida,"ameeleza Mwenyekiti.

Aidha,moja ya tabiri kubwa ni pamoja ya kumuonya aliyekuwa rais wa Zambia Levi's Mwanawasa mwaka 2006 kuwa atashinda uchaguzi mkuu Zambia mwaka 2006 lakini hatokaa sana madarakani jingine ni kumwombea aliyekuwa rais wa Zambia,Frederick Jacob Titus Chiluba kushinda kesi na akashinda pamoja na kumwandikia hayati rais Dkt. John Pombe Magufuli kuwa alikuwa akiona ana maisha kama ya Mwanawasa kama hatoombewa na yeye.

Pia amewatabiria viongozi wengi wakashinda uchaguzi akiwemo aliyekuwa Rais wa Awamu ya Nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiwa Waziri wa Mambo ya Nje mwaka 2004 na Hayati Michael Sata aliyekuwa rais wa Zambia na Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na wengine wengi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news