Rais Samia atoa Bilioni 1.3/- kukamilisha mradi wa maji Dodoma

NA MWANDISHI MAALUM

SERIKALI imetoa kiasi cha Shilingi bilioni 1.3 ili kukamilisha mradi wa maji kwa wakazi wa Njendengwa, Ihumwa, Nzuguni, Nyumba mia tatu, Iyumbu, soko kuu la Ndugai na FFU jijini Dodoma.

Hayo yamesemwa leo Jumatatu tarehe 30 Agosti 2021 na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso alipofanya ziara ya kutembelea maendeleo ya utekelezaji wa mradi wa maji wa Ihumwa Njedengwa wenye thamani ya Sh. bilioni 2.7.

Mradi huo unatekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi waMazingira Mjini Dodoma (DUWASA).
Waziri Aweso amesema, Rais Samia Suluhu Hassan ametoa shilingi Bilion 1.3 kwaajili ya kukamilisha mradi huo na ununuzi na usimikaji wa pampu kubwa mbili za kusukuma maji.

Pia, ulazaji wa mabomba ya kupeleka maji kwenye tenki lenye urefu wa KM11.6, ulazaji wa mabomba ya kusambazia maji yenye urefu wa Km 5.6 kwenda maeneo ya Iyumbu, Njedengwa na Mwangaza, Nyumba 300, FFU, Standi Kuu ya mabasi, Soko la Job Ndugai na eneo la Nzuguni.

Waziri Aweso amewataka DUWASA kuongeza nguvu mara moja pindi watakapopata fedha hizo ili kazi ikamilike ndani ya miezi miwili kuanzia sasa na wananchi waanze kupata maji.

Amesema awali serikali ilitoa shilingi bilioni 1.4 kwa lengo la kuifanya makao makuu ya nchi Dodoma kuondokana na changamoto ya majisafi ambayo ilikuwa ikiwakabili wananchi.

"Tunajua serikali inayoongozwa na Mama yetu mpendwa Samia Suluhu Hassan ni serikali ambayo inawajali wananchi wa hali ya chini. Pamoja na kuwajali watu wa hali ya chini inakusudia kumtua mama ndoo kichwani," amesema Waziri Aweso

"Kwa maana hiyo mama yetu Samia ameona ni vyema kuwawezesha wakazi wa Dodoma ambako ni makao makuu ya nchi, shikingi bilioni 2.7 kwa ajili ya usambazaji wa maji katika maeneo haya," amesmea.

Naye Mkurugenzi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Dodoma (DUWASA), Mhandisi Aron Joseph amesema mradi huo pamoja na kuwa umefikia hatua mzuri lakini changamoto ni kuwepo kwa miamba wakati wa uchimbaji wa mitaro ya utandazaji wa mabomba.

Amesema watatekeleza maagizo ya Waziri Aweso ili kuhakikisha adhima ya Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan ya kumtua ndoo mama kichwani inafikiwa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news