Simba SC:Kila la heri Luis Miquissone

Uongozi wa Simba umemtakia heri na mafanikio mchezaji Luis Miquissone baada ya kujiunga na klabu Al Ahly ya Misri. 

Simba inashukuru kwa mchango wake ndani ya kikosi chetu na akiwa nasi amefanikiwa kutwaa mataji mawili ya Ligi Kuu, mataji mawili ya FA, na Ngao ya Jamii mara moja na tuzo binafsi kama mchezaji bora wa mwezi mara kadhaa.
Simba inaamini Luis ataendelea kufanya vizuri akiwa na timu yake mpya kutokana na uwezo mkubwa alio nao pamoja na nidhamu ya ndani na nje ya uwanja.

Tunaamini Luis ataendelea kuwa mwanafamilia na Balozi wa Simba siku zote.

Imetolewa na Idara ya Habari na Mawasiliano
Simba Sports Club
Agosti 26, 2021

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news