TPDC yatangaza fursa za ajira na biashara bomba la mafuta Geita

Na Robert Kalokola,Diramakini Blog

Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) limewataka wananchi na wafanyabiashara wa Mkoa wa Geita kuchukua fursa mbalimbali ambazo zinapatikana kutokana na ujio wa ujenzi wa Bomba la Mafuta Ghafi ambalo litapita katika Wilaya mbili ya Chato na Mbogwe katika Mkoa wa Geita kutoka Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga.
Wakuu wa idara na maafisa waandamizi kutoka Mkoa wa Geita wakiwa kwenye semina kuhusu Bomba la Mafuta na fursa zake katika mkoa wa Geita iliyoendeshwa na TPDC katika ukumbi wa EPZA mjini Geita.(Picha na Robert Kalokola).

Bomba la kusafirisha mafuta ghafi linaanzia Hoima nchini Uganda hadi Bandari ya Tanga ambalo litapitia katika mikoa minane ya Tanzania Bara ikiwa ni Kagera,Geita ,Shinyanga,Tabora,Singida,Dodoma,Manyara na Tanga.

Hayo yamesemwa na Mratibu wa Mradi wa Bomba la Mafuta kutoka TPDC, Asiadi Mrutu katika semina kwa wakuu wa idara na maafisa waandamizi kutoka Mkoa wa Geita iliyofanyika katika ukumbi wa Kituo cha Uwekezaji Mjini Geita (EPZA) iliyokuwa na lengo la kutoa elimu ya kuufahamu mradi pamoja na fursa zinazo patikana kutokana na mradi huo.

Amesema kuwa, bomba hilo linapita katika mkoa wa Geita kwenye eneo lenye urefu wa kilomita za mraba 169.06 na wakati wa ujenzi fursa zitakazo kuwepo ni pamoja na kusafisha eneo la mradi eneo la mita za mradi 2,400,000,kuchimba mtaro wa bomba (2,064,000),kufukia mtaro(2,064,000),zege(8,600),ujenzi wa uzio (5,000) na kulaza bomba (1,147).
Mratibu wa Mradi wa Bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga, Asiadi Mrutu akitoa mada katika semina ya fursa za Bomba la mafuta katika ukumbi wa EPZA mjini Geita. (Picha na Robert Kalokola).

Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Geita, Herman Matemu amewataka wananchi kuchangamkia fursa hizo zitakazopatikana kutokana na Bomba la Mafuta kupita katika mkoa huo kwa kuajiriwa kufanya kazi lakini pia kwa wafanyabiashara kutoa huduma mbalimbali za kibiashara.
Kaimu katibu Tawala mkoa wa Geita, Herman Matemu akifungua semina ya fursa za Bomba la mafuta mkoa wa Geita katika ukumbi wa EPZA iliyoendeshwa na TPDC. (Picha na Robert Kalokola).

Aidha amesema serikali katika mkoa huo itashirikiana na TPDC kuakikisha miundombinu yote ya Bomba hilo la mafuta inakuwa salama muda wote na kuwataka wananchi kutojaribu kwa namna yoyote ile kuchezea miundombinu ya bomba hilo.

Asiadi Mrutu amefafanua kuwa katika kutekeleza shughuli hizo watu mbalimbali watatakiwa kuajiriwa kwa ajili ya kufanya kazi hizo ikiwemo wataalam kutoka makundi ya uchomeleaji na ujenzi ili kuweza kufanya kazi kwa ufanisi.

Mratibu wa maradi huo, Asiadi Mrutu ametaja fursa nyingine kuwa ni Kukunja vipande mabomba,kuchomelea viungo vya mabomba,huduma ya vinywaji na vyakula kwa wafanyakazi,huduma za matibabu,huduma za usafirishaji wa mizigo pamoja na pamoja na kukodisha mitambo ya ujenzi.
Washiriki wa semina watifuatilia mada katika ukumbi wa EPZA. (Picha na Robert Kalokola).

Aidha,amesema kuwa katika ujenzi wa Bomba hilo kutakuwa kambi mbili ambazo zitakuwa katika Wilaya ya Chato ambako itajengwa Kambi namba 7 na Wilaya ya Bukombe itajengwa Kambi namba 8 na katika ujenzi wa kambi hizo fursa zitakazo patikana kwa wananchi na wafanyabiashara ni Kusafisha eneo lenye ukubwa wa mita 350 kwa 500,vifaa vya ujenzi ikiwemo sementi, mchanga, nondo, kifusi na moramu.

Fursa nyingine alizotaja ni ujenzi wa kambi za kuishi Wafanyakazi zaidi ya 1000,huduma za ulinzi ,huduma za vyakula kwa wafanyakazi zaidi ya 1000 pamoja na na uduma za Mawasiliano ambazo zinatakiwa kutolewa na wafanyabishara wa maeneo husika au kutoka ndani ya nchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news