WAKANDARASI WANAWAKE WATAKIWA KUJITUMA

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Meneja wa Bodi ya usajili wa Wakandarasi (CRB), kanda ya Mwanza Mkadiriaji Majenzi Godfrey Kazi amesema Serikali itazielekeza taasisi nunuzi zote kutenga kazi kwa makundi maalum wakiwepo wanawake ili kuwezesha usawa katika miradi ya ujenzi wa barabara nchini.
Baadhi ya wahitimu wa mafunzo ya wakandarasi wanawake wanaotumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika ujenzi wa barabara wakisikiliza hotuba ya Mgeni rasmi ambaye ni Meneja wa Bodi ya Wakandarasi (CRB), kanda ya Mwanza Mkadiriaji Majenzi, Godfrey Kazi kabla ya kufunga mafunzo hayo Jijini Mwanza.
Meneja wa Bodi ya Wakandarasi (CRB), kanda ya Mwanza Mkadiriaji Majenzi, Godfrey Kazi akimkabidhi cheti cha uhitimu wa mafunzo ya teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika ujenzi wa barabara mhitimu Prisila Kapinga kutoka mkoa wa Geita.

Akifunga mafunzo ya wiki mbili ya wakandarasi wanawake wanaotumia teknolojia stahiki ya nguvukazi katika ujenzi wa barabara jijini Mwanza Meneja huyo amesisitiza umuhimu wa wakandarasi wanawake kufanyakazi kwa bidii na nidhamu ili wapewe miradi mingi na hivyo kukuza katika fani ya ukandarasi.

“Napenda kuwahakikishia kuwa Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi (Sekta ya Ujenzi), imedhamiria kuhakikisha wanawake wanashiriki kikamilifu katika miradi ya ujenzi wa barabara ili kufuata sera zilizopo na kuwakomboa kiuchumi”, amesema mkadiriaji majenzi Kazi.
Meneja wa Bodi ya Wakandarasi (CRB), kanda ya Mwanza Mkadiriaji Majenzi, Godfrey Kazi akimkabidhi cheti cha uhitimu wa mafunzo ya teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika ujenzi wa barabara mhitimu Magreth Robert kutoka mkoa wa Simiyu.
Picha ya pamoja ya Wakandarasi wanawake kutoka Mkoa wa Mara baada ya kuhitimu mafunzo yao ya ukandarasi kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika ujenzi wa barabara yalioandaliwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Jijini Mwanza.

Amesema Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi itaendelea kuhamasisha wanawake kushiriki katika kazi za ujenzi wa barabara ili kuongeza tija kwa wanawake wenyewe na kuondoa dhana kuwa kazi hizo ni kwaajili ya wanaume pekee.

Kwa upande wao washiriki waliohitimu mafunzo hayo wameiomba Serikali kuendelea kuwapa fursa zaidi katika kazi za barabara ili kuwajengea uwezo na kuwawezesha kushiriki kikamilifu katika kukuza uchumi binafsi na wa taifa.
Picha ya pamoja ya Wakandarasi wanawake kutoka Mkoa wa Simiyu mara baada ya kuhitimu mafunzo ya ukandarasi kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi katika ujenzi wa barabara yalioandaliwa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi Jijini Mwanza.

Zaidi ya wanawake 80, kutoka katika mikoa ya Mwanza, Simiyu, Geita, Mara na Kagera wameshiriki katika mafunzo hayo yenye lengo la kuwawezesha wanawake wakandarasi kushiriki katika ujenzi wa barabara kwa kutumia teknolojia stahiki ya nguvu kazi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news