Yanga SC kuanza na River United,Simba na Jwaneng

Yanga SC wataanza na Rivers United ya Nigeria katika Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika Septemba, mwaka huu.

Wanajangwani wataanzia nyumbani kati ya Septemba 10 na 12 kabla ya kusafiri kwenda mjini Port Harcourt kwa mechi ya marudiano ya kati ya Septemba 17 na 19.
Wakifanikiwa kuvuka hapo watakutana na mshindi kati ya Fasil Kenema SC ya Ethiopia na Al Hilal ya Sudan.

KMKM ya Zanzibar yenyewe itaanzia nyumbani dhidi ya Al Itihad ya Libya na ikivuka hapo itakutana na Esperance ya Tunisia.
Mabingwa wa Tanzania, Simba SC wao wataanzia Raundi ya pili ya mchujo dhidi ya mshindi kati ya Jwaneng Galaxy ya Botswana na DFC Beme Arrondissement ya Afrika ya Kati.

Katika Kombe la Shirikisho, Azam FC itaanzia nyumbani dhidi ya Horsed FC ya Somalia, Biashara United itaanzia ugenini dhidi ya FC Dikhil ya Djibouti na Mafunzo ya Zanzibar itaanzia nyumbani dhidi ya Inter Clube ya Angola.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news