Diwani Lyoto awapa walimu,wanafunzi motisha kwa kufanikisha matokeo bora

Na Anneth Kagenda

WALIMU na Wanafunzi katika Shule tatu mbili zikiwa ni za msingi Mzimuni na Mikumi pamoja na ile moja ya Sekondari ya Mzimuni wamepewa motisha ya zawadi mbalimbali zikiwemo fedha taslimu kwa madai kuwa mwaka 2020 walifanya vizuri kwenye mitihani katika Kata ya Mzimuni.
Motisha hiyo imetolewa jijini Dar es Salaam na Diwani wa Kata ya Mzimuni Jimbo la Kinondoni, Manfred Lyoto na kusema kuwa ameamua kufanya hivyo kutokana na kwamba pamoja na mambo mengine ila kipaumbele chake kikubwa kiopo kwenye elimu.

Diwani Lyoto, wakati wa hafra hiyo fupi aliwakabidhi walimu waliofanya vizuri kwenye kuwafundisha watoto na badaye wanafunzi hao wakaweza kufanya vizuri kwenye mitihani yao mwaka jana hivyo walimu hao walikabidhiwa kitita cha fedha kila mmoja sh. 50,000.

Aidha, kwa upande wa wanafunzi waliofanya vizuri walipewa zawadi za peni na madaftari wale waliofanya vizuri kwenye mitihani ya Taifa ya darasa la nne, kidato cha pili na wale wa kidato cha nne mwaka jana.

Diwani huyo alisema kuwa siyo kwamba wengine hawafanyi vizuri bali ameona kuna umuhimu wa kuanza na walimu wachache pamoja na wanafunzi na kwamba wengine wataendelea kufanyiwa utaratibu wa motisha pia.

"Siyo kwamba nyie wengine hamfanyi vizuri hapana hivyo endeleeni kuweka bidii kubwa kwenye ufundishaji watoto lakini pia niwaombe wanafunzi nanyi jitahidini sana madarasàni na muwasikilize walimu wenu wakati sisi wazazi tukiendelea kuwafanyia taratibu mbalimbali za kuwawekea mazingira mazuri," alisema Diwani Lyoto na kuongeza;

"Lakini pia bado tunayo changamoto ya uzio ambayo tunaendelea kuishughulikia kwa haraka, kuhusu chakula tutaendelea kushirikiana na wazazi ili kujua jinsi tutakavyo litatua nalo kwa haraka,".

Alisema pia changamoto nyingine ni ile ya uchache wa walimu wa Sayansi na kwamba amejipanga kuhakikisha walimu hao wanapatikana kutokana na kwamba dunia mzima inaongozwa na walimu ambao ndio wanafanya kazi kubwa ya kuwafundisha watoto ili waweze kufuta ujinga.

"Lakini pia bado tunatatizo la madawati ambalo nalo pia naendelea kulishughulikia ambapo awali nilileta madawati 400 kwa shule ya Mzimuni Sekondari, lakini pia kuna mengine 200 yanakuja na mengine pia yanaandaliwa," alisema.

Hata hivyo alisema kuwa ni vyema walimu kwa nafasi zao wakaendelea kuongeza bidii kwenye ufundishaji watoto lakini pia kujikinga na janga kubwa la Covid 19 kwa kunawa mikono na kuvaa barakoa.

Baadhi ya walimu waliopata motisha hiyo akiwemo Mwalimu wa Tunu Pazzy, Mwalimu Nestory Morro na Mwalimu Farida Marijani walitoa pongezi zao na kuomba taasisi zingine kuendelea kujitolea zaidi kama alivyofanya Diwani Lyoto.

Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mzimuni mwalimu Yahya Kirondo alimshukuru diwani huyo na kumuomba aendelee kujitolea zaidi kutatua changamoto za shule hizo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news