Wezi waisababishia TANESCO hasara ya milioni 65/- Geita

Na Robert Kalokola, Diramakini Blog

Shirika la Umeme (TANESCO) Mkoa wa Geita limepata hasara ya zaidi ya shilingi Milioni 65 kwa kipindi cha miezi 12 zilizotumika kukarabati Transfoma 50 baada wezi kuiba vipuri vyake na kusababisha uharibifu.
Afisa Mahusiano Tanesco Mkoa wa Geita, Emma Nyaki akizungumza na Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja na Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani walipotembelea banda Tanesco katika maonyesho ya Utalii na biashara wilayani Chato. (Picha na Robert Kalokola).

Hayo yameelezwa na Afisa Mahusiano wa TANESCO mkoani Geita, Emma Nyaki alipokuwa akizungumuza na waandishi wa habari kuelezea changamoto zinazoathiri huduma za umeme kwa wateja wa shirika hilo katika Mkoa wa Geita.

Nyaki amesema, wezi wa vifaa vya transfoma wamekuwa wakiharibu miundombino hiyo ya umeme na kusababisha kukatika kwa umeme hali inayowafanya wateja kukosa huduma na kuilazimisha TANESCO kutumia pesa nje ya bajeti ili kurejesha huduma ya umeme.

Afisa Mahusiano Nyaki amesema hayo wakati wa maonyesho ya Utalii na biashara yaliyofanyika katika Wilaya vya Chato ambapo TANESCO ilionyesha huduma zinazotolewa na shirika hilo kwa wananchi.

Ametoa rai kwa wananchi kutoa ushirikiano kwa TANESCO kwa kufichua watu hao ambao wanaharibu miundombinu ya shirika hilo na kusababisha hasara lakini na kukosesha huduma kwa wananchi.
Afisa masoko wa Tanesco Makao makuu Innocent Lupenza akitoa ufafanuzi wa huduma za shirika hilo kwa Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mary Masanja alipotembelea banda la maonyesho la Tanesco Wilayani Chato. (Picha na Robert Kalokola).

"Tunaomba endapo wananchi wataona mtu asiye mwaminifu anakaribia miundombinu ya Tanesco, na siyo mhusika, watoe taarifa, na bahati nzuri maeneo yote ya vijijini tumepita, tumeacha namba za mawasiliano ziweze kutusaidia kutatua changamoto hii," amesema.

Nyaki alitaja changamoto nyingine inayotia hasara shirika hilo katika Mkoa wa Geita ni uchomaji moto wa nguzo za umeme ambapo ndani ya mwaka huu kwa wilaya ya Chato pekee shirika hilo mkoani limetumia takribani sh.milioni 11 kubadilisha nguzo zilizounguzwa.

Amesema kutokana na nguzo kuchomwa moto, mnyororo wa hasara ni mrefu kwani shirika linapata hasara,lakini mteja anakosa umeme,na wale wanaopata huduma mbalimbali Kama biashara kwa kutegemea umeme wanakosa riziki zao.

Katika maonyesho ya utalii na biashara yaliyofanyika katika Wilaya ya Chato,banda la TANESCO limetembelewa na watu mbalimbali kwa ajili ya kujifunza huduma zinazo tolewa na shirika hilo.
Afisa Mahusiano Tanesco Mkoa wa Geita Emma Nyaki akizungumza na Naibu waziri wa Maliasili na Utalii Mary Masanja na Waziri wa Nishati, Dkt.Medard Kalemani walipotembelea banda Tanesco katika maonyesho ya Utalii na biashara Wilayani Chato.(Picha na Robert Kalokola).

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news