Anord Mtei kizimbani kwa tuhuma za kufyeka nyeti za mwenzake

Na Hadija Bagasha, Tanga

Anord Mtei ambaye ni mkazi wa Kijiji cha Kilindi asilia amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Wilaya ya Kilindi akikabiliwa na tuhuma za kumfyeka mwenzake sehemu za siri.
Akimsomea mashitaka yake mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Kilindi, Mariam Mfanga, mwendesha mashitaka wa mahakama hiyo, Cpl Seif Makono alieleza kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo katika kijiji cha Kilindi asilia.

Cpl Makono alieleza kuwa, mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo Julai 29,mwaka huu na kwamba alimkata Matonya Luberege sehemu zake za siri kwa kutumia kitu chenye ncha kali.

Alidai kuwa kitendo hicho kilimsababishia mlalamikaji wa kesi hiyo maumivu makali mwilini mwake.

Adidai kuwa, kitendo alichokifanya mshitakiwa ni cha kikatili na ambacho pia ni kosa na kinyume na sheria.

Hata hivyo mshitakiwa alikana shitaka hilo na kurejeshwa rumande baada ya kukosa watu wa kumdhamini.

Kesi hiyo imepangwa kuja mahakamani hapo kwa mara ya pili kwa ajili ya kuanza kusikilizwa Septemba 24, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments