Mtenga: Kamati imewasikiliza na kuwahoji wabunge watatu CCM

Na Doreen Aloyce, Diramakini Blog

KAMATI ya Maadili ya wabunge imemaliza kuwahoji wabunge watatu Josephat Gwajima Mbunge wa Jimbo la Kawe, Jerry Silaa Mbunge wa Jimbo la Ukonga na Mbunge wa kuteuliwa Humphrey Polepole.
Akiongea mara baada ya kumalizika kwa mahojiano hayo, Hassan Mtenga ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili na pia Mbunge wa Mtwara Mjini amesema wameanza kikao hicho mnamo majira ya saa 2 asubuhi ambapo kamati hiyo imewasikiliza na kuwahoji wabunge hao.

"Tumewasikiliza kama kamati na sisi pia tutakwenda kuwasilisha taarifa za mahojiano haya kwenye kamati ya uongozi wa bunge ambayo mwenyekiti wake ni Kassim Majaliwa, Mbunge wa Jimbo la Ruangwa," amesema Mtenga.

Hata hivyo, mahojiano hayo yalianza majira ya saa 2 asubuhi ambapo wa kwanza kuhojiwa alikuwa ni Humphrey Polepole aliyewasili mapema katika viwanja vya CCM makao makuu.

Wa pili kuhojiwa na kamati hiyo alikuwa ni mbunge wa Jimbo la Ukonga,Jerry Silaa ambapo aliwasili na kwenda kuhojiwa majira ya saa 5 na nusu asubuhi na kutoka majira ya saa 6 :27 mchana.

Na wa mwisho kuhojiwa alikuwa Mbunge wa Kawe,Askofu Josephat Gwajima ambaye alihojiwa kuanzia saa 6:28 mchana na kutoka saa 8 na dakika 20 mchana.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news