Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba amtabiria Freeman Mbowe makubwa

NA MWANDISHI MAALUM

Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa, Alphonce Temba ameingia katika Gereza la Ukonga lililopo jijini Ilala, Dar es Salaam na kumtabiria, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Taifa, Freeman Mbowe makubwa.
Temba ambaye aliongozwa na Roho Mtakatifu kwenda gerezani humo, amesema, Mungu anakwenda kufanya jambo na punde mambo yatakaa sawa.

Mwinjilisti Temba ambaye aliongea na Mbowe katikati ya ulinzi mkali aliwapigisha maombi makali na kuzama katika ulimwengu wa Roho ndipo kwa mara ya kwanza alijitambulisha kwa mwenyekiti Mbowe na kumpa unabii wa chama chake na yeye mwenyewe, hata hivyo alimshuhudia safari yake ya Zambia na Botswana na kumweleza maono ambayo Mungu alimletea Septemba 17, 2021.

Amemweleza kuwa,kuna kusudi jema ambalo Mungu ameweka ndani yake, hivyo asife moyo kwa maana Mungu alimuonyesha, Mbowe alilazimika kupita katika bonde la mauti, lakini baada ya maombi maalum, Mungu anakwenda kutenda mambo makuu karibuni.

Mwinjilisti Temba amesema alichomwambia Mungu juu ya Mbowe hakuna mamlaka yoyote inayoweza kuingilia kati ambapo baada ya ujumbe huo maalum wa kinabii kutoka kwa Mwinjilisti Temba, Mheshimiwa Freeman Mbowe alimwaga machozi na kushukuru.

Hata hivyo, Mwinjilisti alimweleza Mbowe atakayeingilia mpango wa Mungu kwa kumuonea Mbowe atapatwa na mauti ya ghafla, hivyo yeye angaliye na aandike tarehe aliyowasilisha ujumbe huo na ajue nabii kaingia gerezani.

Aidha, baada ya kutoka baadhi ya mafisa magereza walikuwa wakiomba maombi binafsi na utabiri na wakatabiria kadri Roho Mtakatifu alivyomuongoza.

Mwinjilisti Temba kati ya matukio ambayo Mungu amemtumia katika mambo makubwa ni pamoja na kumtabiria na kumuombea aliyekuwa rais wa Zambia, Frederick Jacob Titus Chiluba ambapo mwaka 2004, Mungu alimtuma kwenda Zambia nyumbani kwake Kabulonga kumuombea na kuifuta kesi iliyokuwa inamkabili chini ya utawala wa rais wa kipindi hicho,Levy Patrick Mwanawasa mwaka 2006 ambapo alimtabiria Rais Mwanawasa kuwa angeshinda Uchaguzi wa mwaka huo.
Lakini asingedumu katika Urais wake baada ya kifo cha Mwanawasa, Mwinjilisti Temba alifunguliwa na Mungu juu ya kiongozi wa upinzani nchini Zambia wa chama Cha PF, Michael Satta kuwa angekuwa rais baadaye na akafanikiwa kushinda urais.

Hivi karibuni, Mwinjilisti Temba alitabiri ushindi wa chama cha upinzani nchini Zambia na alikuwa miongoni mwa wageni waalikwa, mwaliko kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama tawala nchini Zambia (UPND) Taifa, Stephen Katuka kilichomwingiza madarakani,Hakainde Hichilema.

Pia Muhubiri na Mwinjilisti wa Kimataifa wa Kanisa la Penuel Healing Ministry la Ubungo Kibangu jijini Dar es Salaam, Alphonce Temba pia Kamati ya Viongozi wa dini nchini Zambia imempendekeza kuwa miongoni mwa washauri wa rais.

Baada ya kutoka Zambia, Mwinjilisti Temba aliitwa Ikulu ya Botswana na kukutana na Waziri anayehusika na Masuala ya Rais, Utumishi na Utawala wa Umma, Mheshimiwa Kabo Neale Sechele Morwaeng.

Akizungumza baada ya kuwasili Botswana, Mwinjilisti Temba amesema, ameendelea kuitikia wito wa Mungu wa kwenda kutamka neno la uponyaji na ushindi kwa mataifa mbalimbali Kusini mwa Afrika.

Maombi yanaweza kuwa silaa tosha. Ikizingatiwa kuwa, Botswana walifungia watu ndani na kila wiki waligawa chakula nyumba zote nchi nzima na nusu ya wananchi wamechanjwa, lakini imekuwa na vifo vingi ikifuatiwa na India kwa sasa kulingana na takwimu za mara kwa mara.

"Ninamshukuru Mungu, baada ya kuingia Ikulu na kupokelewa na Waziri Ofisi ya Rais, Mheshimiwa Kabo baada ya maongezi pamoja na washauri wa rais wakakubaliana nami kuwa sasa Botswana kwa mara ya kwanza Serikali iitishe maombi ya mwezi mzima kumlilia Mungu.

"Kusudi Mungu aponye nchi na vizuizi viachilie. Jambo hilo limeleta mjadala sana kutoka baadhi ya madhehebu hapa kuwa, kwa nini mtumishi mgeni toka Tanzania atumike kuanzisha maombi, lakini Bwana akaingilia kati na maombi yanaendelea.

"Nawashukuru watanzania kwa maombi yenu, lakini kilichoniletea heshima zaidi ni kwa sababu ya Hayati Rais Dkt.John Pombe Magufuli,kwani wakati korona ilipoingia nchini, mara ya kwanza na kuwatangazia watanzania na Dunia kuwa Mungu atatuondolea korona mmoja wa mbunge wa Botswana katika Bunge aliomba Bunge kutoa kauli ya maombi, lakini Makamu wa Rais hapa akaipinga na kudai wako kwenye jambo zito na maombi hayana nafasi katika hilo.

"Ndipo hali ikazidi kuwa mbaya zaidi kwa mujibu wa takwimu za Dunia walikuwa wanaongoza,kila leo mpaka Mungu alivyonileta kuitisha maombi ya Kitaifa,Mungu apewe sifa na utukufu, na mataifa na wenye mamlaka kudharau maombi katika mataifa yao mwisho ni aibu na fedheha,"amesema Mwinjilisti Temba.

Aidha, baada ya maombi ya Mwinjilisti Temba nchini Botswana, ndani ya wiki moja tatizo la mlipuko wa Corona lilipungua katika maambukizi kwa takwimu za ndani na kidunia na shule zikafinguliwa kama vile neno la mtu wa Mungu alivyosema.

Post a Comment

0 Comments