NHIF: Miaka 20,Uhakika wa Matibabu kwa Wote

NA MWANDISHI DIRAMAKINI

Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) umeendelea kurahisisha upatikanaji wa huduma zake ambapo kwa sasa umeanzisha usajili wa wanachama kupitia mtandao.

Aidha, mafanikio hayo yanaenda sambamba na maboresho mengine ya kisasa ambapo mwezi Oktoba, mwaka huu watafanya kilele cha miaka 20 ya mfuko huo na watazindua programu tumishi ya Taarifa App, hivyo wenye simu za kisasa wataweza kupata taarifa yoyote iwe ni michango,kituo,aina ya dawa kabla ya kwenda kwenye kituo na hivyo kuweza kupunguza malalamiko kwa wanachama.

Mkurugenzi wa Huduma na Wanachama wa NHIF,Christopher Mapunda ameyabainisha hayo wakati akiwasilisha mada ya miaka 20 ya mfuko ulipotoka,walipo na wanakoelekea wakati wa mkutano na waandishi wa habari nchini na NHIF uliofanyika katika Ukumbi wa LAPF jijini Dodoma.

"Jitihada hizo ni miongoni mwa mafanikio makubwa ya maboresho yetu katika mifumo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ambayo pia yamelenga kuwasaidia watoa huduma kulipwa madai yao moja kwa moja kutoka Hhspitalini kwa lengo la kuondoa ucheleweshwaji wa malipo,"amesema.

Miongoni mwa huduma za kujisajili mtandaoni ni pamoja na kujisajili kupitia vifurushi vya NAJALI AFYA, WEKEZA AFYA, TIMIZA AFYA, kuhuisha uanachama wa Toto Afya pamoja na usajili wa wanafunzi.

Kwa mujibu wa NHIF miongoni mwa mambo muhimu ambayo unapaswa kuyazingatia ili kufanikisha huduma hizo ni pamoja na mwanachama wa vifurushi kutimiza vigezo vifuatavyo.

Mosi ni pamoja na mwanachi anayejisajili katika mpango wa vifurushi anapaswa kuwa na namba ya kitambulisho cha Taifa na namba ya simu ya mkononi.

Pili ni mwananchi anayejisajili pamoja na mwenza wake anapaswa kuwa na namba ya kitambulisho cha mwenza wake na nakala ya cheti cha ndoa.

"Mwanachama anayemwandikisha mtoto kama mtegemezi atahitajika kuambatanisha picha ya mtoto na nakala ya cheti cha kuzaliwa cha mtoto. Tangazo la kuzaliwa linaweza kutumika kama mbadala wa cheti cha kuzaliwa endapo mtoto ana umri chini ya miezi sita,"imeeleza.

Aidha, kwa mujibu wa NHIF, mwanafunzi anayetaka kujisajili anatakiwa kuwa na namba ya utambulisho ya kidato cha nne (Form IV index number), namba ya simu na picha ndogo.

Kwa upande wa TOTO AFYA, NHIF inaeleza kuwa, ili kuhuisha uanachama wa huduma hii, mwanachama tatakiwa kuwa na namna ya kadi ya uanachama ya mtoto na namba ya simu

"Viambatanisho vyote vinavyohitajika ili kukamilisha usajili vinatakiwa kuwa katika nakala laini (sofy copy). Baada ya usajili kukamilika mwanachama atapewa namba ya malipo (control number) kwa njia ya ujumbe mfupi (sms) kupitia simu yake ya mkononi ambayo ataitumia kufanya malipo kupitia benki au mitandao ya simu,"wamefafanua.Jisajili kwa njia ya mtandao,bofya hapa>>>

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news