Rais Samia atengua mawaziri watatu, ateua papo kwa papo

*Kalemani, Ndungulile, Chamuriho 'OUT' , Januari Makamba, Dkt.Tax, Dkt.Kijaji, Prof. Mbarawa 'IN'...Dkt.Feleshi ndiye Mwanasheria Mkuu wa Serikali

NA GODFREY NNKO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan leo Septemba 12, 2021 amefanya uteuzi wa baadhi ya mawaziri na viongozi wengine huku akitengua teuzi.
Miongoni mwa walioteuliwa kuwa waziri ni Mheshimiwa Dkt.Stergomena Lawrence Tax (MB) kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Mheshimiwa Dkt.Tax kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Jaffar Haniu anachukua nafasi ya marehemu Elias John Kwandikwa ambaye alikuwa Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga.Pia unaweza kusoma uteuzi mpya hapa>>>

Wakati huo huo Mheshimiwa, Rais Samia amemteua Mheshimiwa Dkt. Ashatu Kachwamba Kijaji (Mb) kuwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari. Dkt. Kijaji anachukua nafasi ya Dkt. Faustine E. Ndungulile (MB).

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, uteuzi wa Mheshimiwa Ndungulile umetenguliwa. Pia Rais Samia ameihamishia Idara ya Habari katika wizara hii kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo.

Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Rais Samia amemteua Mheshimiwa January Yusuf Makamba (MB) kwa Waziri wa Nishati. Mheshimiwa Makamba anachukua nafasi ya Dkt. Merdard Matogolo Kalemani (Mb) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.Zinazofanana bonyeza hapa>>>

Pia Mheshimiwa Rais Samia amemteua Profesa Makame Mnyaa Mbarawa (MB) kuwa Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi. Mheshimiwa Profesa Mbarawa anachukua nafasi ya Mhandisi Dkt. Leonard Madaraka Chamuriho (MB) ambaye uteuzi wake umetenguliwa.

Rais Samia amemteua Dkt. Eliezer Feleshi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali akichukua nafasi ya Prof. Adelardus Kilangi aliyekuwa Mwanasharia Mkuu wa Serikali ambaye ameteuliwa kuwa Balozi, kabla ya uteuzi huo Feleshi alikuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news